Michezo

GSU na Prisons kujaribu kunyang'anya Waarabu taji voliboli

March 31st, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na GEOFFREY ANENE

WAWAKILISHI wa Kenya katika voliboli ya Klabu Bingwa barani Afrika ya wanaume, GSU na Prisons, wataanza kampeni zao za kutafuta taji dhidi ya Asaria ya Libya na Wolaita ya Ethiopia mnamo Aprili 1, 2019 jijini Cairo, Misri.

Wakenya hawa waliondoka nchini Kenya mapema juma lililopita wakiapa kuwa wagombeaji halisi wa taji. Matokeo mazuri ya timu za Kenya katika voliboli ya wanaume ya Afrika ni medali ya fedha ambayo Prisons ilinyakua jijini Cairo mwaka 2011 nayo GSU ilishinda nishani ya shaba mwaka 2005 nchini Benin. Hakuna klabu kutoka nje ya kaskazini mwa Afrika imewahi kutwaa taji. Makala ya mwaka huu ni ya 38.

MAKUNDI:

Kundi A – Ahly (Misri), AS Injis (Ivory Coast), Police 6 (Botswana), Mugher (Ethiopia), Ahly Tripoli (Libya);

Kundi B – Smouha (Misri), Gisagare (Rwanda), Christian (Uganda), Gendarmarie (Madgascar), Etihad (Libya);

Kundi C –Swehly (Libya), Rukinzo (Burundi), Woliata (Ethiopia), Prisons (Kenya), Espoire (DR Congo), FAP (Cameroon);

Kundi D – GSU (Kenya), University (Zimbabwe), AS Fag (Guinea), Mwangaza(DR Congo), Nemostars (Uganda), Asaria (Libya).

Mwaka Mabingwa

1980 Ahly (Misri)

1983 Ahly (Misri)

1984 Zamalek (Misri)

1985 CS Sfax (Tunisia)

1986 CS Sfax (Tunisia)

1987 Zamalek (Misri)

1988 Mouloudia (Algeria)

1989 CS Sfax (Tunisia)

1990 Nasr Hussein Day (Algeria)

1991 Club Africain (Tunisia)

1992 Club Africain (Tunisia)

1993 Club Africain (Tunisia)

1994 Esperance (Tunisia)

1995 Ahly (Misri)

1996 Ahly (Misri)

1997 Ahly (Misri)

1998 Esperance (Tunisia)

1999 CS Sfax (Tunisia)

2000 Esperance (Tunisia)

2001 Etoile du Sahel (Tunisia)

2002 Etoile du Sahel (Tunisia)

2003 Ahly (Misri)

2004 Ahly (Misri)

2005 Sfax (Tunisia)

2006 Ahly (Misri)

2007 Mouloudia (Algeria)

2008 Zamalek (Misri)

2009 Zamalek (Misri)

2010 Ahly (Misri)

2011 Ahly (Misri)

2012 Zamalek (Misri)

2013 Sfax (Tunisia)

2014 Esperance (Tunisia)

2015 Ahly (Misri)

2016 Al Guish (Misri)

2017 Ahly (Misri)

2018 Ahly (Misri)