• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:07 PM
Harambe Stars yakwama 105 viwango vya FIFA

Harambe Stars yakwama 105 viwango vya FIFA

NA CECIL ODONGO

TIMU ya Taifa Harambee Stars imesalia katika nafasi ya 105 iliyoshikilia mwezi Novemba mwaka 2019 kulingana na orodha iliyotolewa na Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA mnamo Alhamisi Disemba 20, 2019.

Kenya ilijizolea alama 1210 kulingana na matokeo hayo ya FIFA, hii ikiwa ni alama sawa iliyopata mwezi Novemba.

Katika bara Afrika, timu ya taifa ya Senegal maarufu kama ‘The Lions of Teranga inaongoza huku ikishikilia nafasi ya 23 duniani kwa alama 1505.

Timu ya Taifa ya Uganda kwa jina Uganda Cranes pia hawakusonga hata hatua moja kwa kuwa bado wanashikilia nafasi yao ya awali ya 75 duniani kwa alama 1320.

Hali sawa na hiyo iliwakuta Ghana ambao ni  wapinzani wa Kenya kwenye mechi zinazoendelea za kufuzu kushiriki Taifa bingwa la Bara Afrika(Afcon) mwaka wa 2019.  Black Stars wapo katika nafasi ya 51 ulimwenguni, nafasi waliyoshikilia mwezi Novemba.

Majirani Tanzania wapo katika nafasi ya 138 kwa alama 1087 nao Misri wanaoshikilia nafasi ya saba barani Afrika wakiwa nambari 56 duniani.

Hata hivyo soka ya mabingwa wa Afcon mwaka 2012 Zambia inaendelea kuzorota baada ya vigogo hao wa zamani kuporomoka hadi nafasi ya 83 kwa alama 1292. Zambia tayari wamebanduliwa nje ya kipute cha mwaka wa 2019.

Taifa la Ubelgiji ndilo bora zaidi duniani ikifuatwa na Ufaransa, Brazil, Croatia, Uingereza, Ureno na Uruguay katika uchanjari huo.

Washindi wa Kombe la Dunia mwaka wa 1988 na 2014 Argentina na Ujerumani hata hivyo wanaendelea kudhoofika kigozi  baada ya kuorodheshwa nje ya mduara wa mataifa kumi bora. Argentina wapo katika nafasi ya 11 huku Ujerumani wakishikilia nafasi ya 16.

  • Tags

You can share this post!

AFYA: Changamoto ilizopitia Hospitali ya Bondeni kuimarisha...

Wafamasia walia kutengwa katika uundaji wa bodi

adminleo