• Nairobi
  • Last Updated May 11th, 2024 3:59 PM
Hii imeenda? Liverpool sasa waanza kunusa ubingwa wa EPL

Hii imeenda? Liverpool sasa waanza kunusa ubingwa wa EPL

LONDON, Uingereza

HUU ukiwa msimu unaotarajiwa kusajili mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Liverpool wamekamata usukani kwa nguvu wakiwa na nia ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Baada ya timu hiyo kuagana na mastaa muhimu wakiwemo Fabinho na Jordan Henderson, japo kocha Jurgen Klopp alijaza nafasi hizo, wengi hawakutarajia timu hiyo kuwa kileleni mwa jedwali kufikia Januari 1, 2024.

Liverpool inaongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 45 baada ya kushindwa mara moja tu katika mechi 20 tangu msimu huu uanze.

Ushindi wao wa mabao 4-2 dhidi ya Newcastle United katika mechi iliyochezwa Jumatatu umewakitisha zaidi uongozini kwa pengo la pointi tatu mbele ya Astona Villa walio na pointi 42. Lakini wako pointi tano mbele ya mabingwa watetezi Manchester City walio na mechi moja mkononi pamoja na Arsenal.

“Huo ndio mchezo waliocheza vizuri zaidi tangu msimu huu uanze,” alisema mlinzi wao wa zamani Jamier Garragher kupitia Sky Sports.

Kumekuwa na misimu mingi ya ligi hii, lakini hakuna mchezo ninaoweza kulinganisha na jinsi waliovyocheza leo (Jumatatu), hasa wakati huu ambapo timu nyingi zinapigania taji.”

Mbali na mabao mengi waliyofunga, Liverpool walikuwa na nafasi 34 za kufunga lakini wakapoteza nyingi.

Walikuwa na nafasi 18 za wazi katika kipindi cha kwanza, ikiwemo penalti lakini timu hizo zilienda mapumzikoni zikiwea sare ya 0-0. Gwiji wao Mohamed Salah alipoteza mkwaji huo.

Hatimaye, Liverpool ilipata ushindi baada ya kufunga matatu katika muda usiozidi dakika 15 huku kocha Klopp akisifu vijana wake kwa kucheza kwa kiwango cha juu.

“Tulianza kwa kishindo. Kila mtu alicheza vizuri. Ni mchezo ambao vijana wanaoibukia wanapaswa kuutazama mara kwa mara. Kila kitu kilikuwa sawa.”

Salah alifunga mabao mawili katika mchezo huo, licha ya mvua kubwa iliyonyesha Merseyside mechi ikiendelea.

Raia huyo wa Misri sasa atajiunga na kikosi cha taifa kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika nchini Ivory Coast mwezi huu, ambapo itabidi mtu mwingine ajaze nafasi yake wakati michuano hiyo ikiendelea kati ya Januari 13 na Februari 11, 2024.

Alifunga bao la kwanza dakika ya 49 kabla ya Alexander Isak kusawazisha dakika tano baada ya kuandaliwa pasi na Anthony Gordon.

Vijana wa Klopp waliendelea kufanya mashambulizi langoni na kufanikiwa kupata bao kupitia Curtis Jones, kabla ya Cody Gapko kuongeza la tatu dakika za 74 na 78 mtawalia.

Newcastle United walipata bao la pili kupitia kwa Sven Botman aliyefunga mpira wa kona dakika ya 81 na kufanya mambo kuwa 3-2 kabla ya Salah kumimina wavuni bao la nne dakika ya 86 baada ya kumchanganya kipa matata Martin Dubravka.

Liverpool hawajashindwa nyumbani msimu huu, wakijivunia ushindi mara nane na sare mbili.

  • Tags

You can share this post!

Papa Francis aitisha mazungumzo maaskofu wakiendelea...

Mwanafunzi fisi akosa ufadhili kwa kubainika anapenda sketi...

T L