Michezo

HOFU YA OLIMPIKI: Wanariadha wahofia afya zao

March 19th, 2020 Kusoma ni dakika: 2

Na MASHIRIKA

TOKYO, Japan

HATUA ya waandalizi wa Michezo ya Olimpiki ya 2020 (IOC) kutofutilia mbali mashindano hayo imeanza kuwatia wanariadha kiwewe.

Baadhi ya wanamichezo wamesema kwamba hatua hiyo inahatarisha maisha yao.

Michezo hiyo imepangwa kuanza Julai 24 licha ya shughuli nyingi za michezo kupigwa marufuku kote duniani kufuatia janga la corona.

Bingwa wa Olimpiki Katerina Stefanidi alisema Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) “inahatarisha afya yao.”

Naye Katarina Johnson-Thompson wa Uingereza alidai hata shughuli za maandalizi zimevurugwa kwa kiasi kikubwa.

Lakini IOC ilijibu ikisema: “Hii si hali isiyo ya kawaida inayohitaji kufanyiwa maamuzi ya kipekee huku tukizingatia maisha ya wanariadha, tukitafuta mbinu za kuwazuia kujipata hatarini kiafya.

“Hakuna hatua itakayochukuliwa haraka kufuatia vilio vya wanariadha, hapa tutategemea wanariadha watakaojitolea kuhakikisha wameshiriki,” Johnson-Thompson aliendelea.

Ni siku chache zilizobakia kabla ya mashindano haya kuanza, lakini kwa hakika wanariadha wamekumbwa na hali ngumu, kuanzia kwa maandalizi. Bingwa huyo wa Dunia katika mashindano ya heptathlon anajiandaa kurejea Uingereza baada ya kujiandalia nchini Ufaransa ambako alidai kila kitu kinatarajiwa kufungwa rasmi.

Waandalizi wa Tokyo 2020 wameahidi kuandaa michezo kwa kiwango cha juu, lakini mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 27 amedai kamati ya IOC imechanganya wetu wengi kuhusu uandalizi huo.

Alisema, “IOC inaendelea kuwasihi wanariadha wazidi kujiandaa kwa ajili ya michezo hiyo huku ikibakia miezi michache tu, wakati mataifa mengi yamezuia watu kutangamana, huku kambi nyingi za mazoezi na hata viwanja vya umma vikiendelea kufungwa.

“Kwa sasa, nina presha nyingi na kwa kweli siwezi kujiandaa vyema kama kawaida, kwa sababu mambo yamebadilika. Tayari nimefuzu kushiriki Olimpiki, lakini afya yangu ni muhimu. Itakuwa vigumu kwa wanariadha wengi kuzua upinzani unaofaa kutokana na maandalizi duni.”

Kambi zote za mazoezi, shughuli zote za michezo, mikutano ya hadhara imepigwa marufuku, watu wameonywa kukusanyika, wanariadha hawawezi kujiandaa kwa pamoja hasa nchini Uingereza, Scotland na Wales.

“Afya zetu zimo hatarini,’’ alisema mwanariadha huyo ambaye ameungwa mkono na wenzake wengi kuhusu maandalizi duni.

Stefanidi, aliyetwaa nishani ya dhahabu nchini Ugiriki katika shindano la kurusha mkuki kwenye michezo ya Olimpiki za Rio mnamo 2016.

“Kamati ya IOC inataka kutuweka hatarini, afya ya familia zetu pia imo hatarini iwapo tutaendelea kujiandaa kila siku. Kwa kweli wametuweka katika hali ngumu, wakati huu michezo inakaribia kuanza,” akasema Johnson-Thompson. Uingereza ni miongoni mwa mataifa yaliyohadharisha raia wake kuhusu mikutano ya hadhara kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Akitangaza tahadhari hizo, Waziri Mkuu wa taifa hilo, Boris Johnson alisema hatua hiyo ipapaswa kuchukuliwa kama tahadhari juu ya maambuliki ya ugonjwa huo hatari.

Aliongeza kwamba kambi za starehe, zikiwemo baa za burudani ni miongoni mwa sehemu hatari zaidi kwa sasa.