• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 9:11 AM
Ivanovic arejea EPL kusaidia West Brom kuhangaisha wapinzani

Ivanovic arejea EPL kusaidia West Brom kuhangaisha wapinzani

Na MASHIRIKA

KIKOSI cha West Bromwich Albion wamemsajili beki wa zamani wa Chelsea, Branislav Ivanovic kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Serbia aliagana na Zenit St Petersburg mnamo Julai 2020 baada ya kunogesha Ligi Kuu ya Urusi kwa miaka mitatu na nusu.

Akiwa mwanasoka wa Chelsea, Ivanovic aliwajibishwa kwenye jumla ya mechi 377 katika kipindi cha miaka tisa iliyomshuhudia akinyanyua ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), makombe matatu ya FA, TAJI MOJA LA Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) na moja la Europa League.

“Ni nyongeza muhimu zaidi kwetu hasa ikizingatiwa kwamba tunalenga kusuka kikosi kilicho na mseto wa wanasoka chipukizi na wale walio na uzoefu mpana katika EPL,” akasema kocha Slaven Bilic.

“Ivanovic amefanya takriban kila kitu katika taaluma yake ambayo ana kila sababu ya kujivunia. Analeta tajriba pevu kambini mwetu na uongozi unaostahili ndani na nje ya uwanja,” akasema Bilic.

Kwa upande wake, Ivanovic alisema: “Kipute cha EPL ndicho bora zaidi duniani. Nimepania kujipa changamoto mpya na niko tayari kutoa mchango wangu kwa mara nyingine katika kivumbi hiki nikivalia jezi za West Brom.”

 

TAFSIRI: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Mabunge mawili ya kitaifa sasa yalegeza masharti ya corona

Wasanii wacheshi wakwama mitandaoni kujikimu kimaisha