• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Jericho yaanza kutetea taji la Super 8 Premier League

Jericho yaanza kutetea taji la Super 8 Premier League

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya Jericho Allstars imeshinda Metro Sports kwa bao 1-0 na kuanza kufufua kampeni zake kutetea taji la Super 8 Premier League (S8PL) kwenye mechi iliyochezewa uwanjani Babadogo, Nairobi.

Nayo Lebanon FC ilitoka sare ya mabao 2-2 na Shaurimoyo Sportiff na kuendelea kushikilia nafasi ya pili na tatu mtawalia kwenye msimamo wa kipute hicho. Wachezaji wa Jericho Allstars na wapinzani wao walishusha soka soka safi huku pande zikionekana kutoshana nguvu.

Hata hivyo wachana nyavu wa Jericho Allstars walipigana kwa udi na uvumba na kufanikiwa kuzima ndoto ya wenzao kupitia bao lililofumwa kimiani na Kevin Juma kipindi cha pili.

”Dah! Mechi hiyo kamwe haikuwa mteremko lakini nashukuru vijana wangu kwa kujituma kiume na kuzoa alama zote tatu,” kocha wa Jericho Allstars Thomas Okongo alisema na kudokeza kwamba msimu huu mahasimu wao wamejipanga tayari kuwabomoa michezoni.

Kocha wa Jericho Allstars, Thomas Okongo akiwapa mawaidha vijana wake kwenye mechi za kuwania Super Eight Premier League(S8PL). Jericho ilivuna ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Metro Sports wikendi. Picha/ John Kimwere

Kwenye matokeo hayo, Makadara J.L.S.A ilitandika Team Umeme kwa mabao 2-0 kupitia Marvin Wachai baada ya kucheka na wavu mara mbili. Nao Wasomi wa Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Kenya (TUK) walikosa makali na kurandwa kwa bao 1-0 na Dagoretti Former Player.

MATOKEO YA MECHI WIKENDI

Lebanon FC 2-2 Shaurimoyo Sportiff

Githurai Allstars 4-2 Rongai Allstars

Team Umeme 0-2 Makadara J.L.S.A

Kawangware United 0-0 Huruma Kona

Dagoretti F.P 1-0 T..U.K

Metro Sports 0-1 Jericho Allstars

MASA 2-1 Mathare Flames

Mashabiki wa Jericho Allstars katika eneo la Jericho wakifuatilia vijana hao walicheza mojawapo kati ya mechi za Super Eight Premier League( S8PL). Picha/ John Kmwere
  • Tags

You can share this post!

Raila alijaribu kuniingiza ‘box’ mara 4 lakini...

Thika Queens wajikuta njia panda KWPL

adminleo