• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 12:11 PM
Juu ya meza KPL ni Tusker, Gor na Ingwe mtawalia

Juu ya meza KPL ni Tusker, Gor na Ingwe mtawalia

Na JOHN ASHIHUNDU

BAADA ya kujitupa uwanjani mara nane, mabingwa wa zamani Tusker wamechukua uongozi wa msimamo wa Ligi Kuu ya Taifa (KPL) baada ya kufikisha pointi 16.

Gor Mahia ambao mwishoni mwa wiki walikuwa ugenini kucheza na DC Motema Pembe wanashikilia nafasi ya pili, licha ya kucheza mechi chache.

Mabingwa hao watetezi wanajivunia jumla ya pointi 15 kutokana na mechi tano, huku wakifuatwa na mahasimu wao wakuu, AFC Leopards ambao pia wamefikisha pointi 15, lakini baada ya kucheza mechi nane.

Kupanda kwa Tusker kulitokana na ushindi wao wa 3-2 dhidi ya Nzoia Sugar katika mechi iliyochezewa Kenyatta Stadium, Machakos.

Vijana hao wa kocha Robert Matano walipata mabao yao kupitia kwa Timothy Otieno (2) huku la tatu likipatikana kupitia kwa Mike Madoya.

Kwingineko, mechi kati ya Mathare United na Posta Rangers ilimalizika bila kufungana, hii ikiwa sare ya tano kwa timu hizo, kila moja ikiwa imejikusanyia pointi 11 ingawa Mathare wamecheza mechi chache.

Wikendi mbaya

Ilikuwa wikendi mbaya kwa kocha William Muluya wa Kariobangi Sharks ambao walichapwa 1-0 na Zoo Kericho, hiki kikipwa kichapo cha tatu kwa vijana hao. Sharks wameshinda mechi moja pekee tangu msimu uanze, baada ya kutoka sare mara nne.

Mechi yao ifuatayo itakuwa dhidi ya limbukeni Kisumu All-Stars ambayo imebakia katika nafasi ya pili kutoka mkiani, mbele ya Chemelil Sugar.

Sony Sugar FC ambao walitolea kwa shida na mabwanyenye Wazito FC ambao waliwachapa kwenye mechi iliyochezewa Machakos.

Mjini Kakamega, Sofapaka waligana kwa kufungana 2-2 na Jumapili katika mechi iliyochezewa Bukhungu Stadium.

 

Matokeo ya wikendi

Mathare United 0-0 Posta Rangers, Wazito FC 4-3 Sony Sugar FC, Tusker FC 3-2 Nzoia Sugar FC, Chemelil Sugar FC 1-1 Kisumu All-Stars, AFC Leopards 0-0 Ulinzi Stars, Kariobangi Sharks 0-1 Zoo Kericho, Kakamega Homeboyz 2-2 Sofapaka FC.

  • Tags

You can share this post!

Jepkosgei amezea kuvunja rekodi ya mbio za marathon

Bayern Munich yafurusha kocha baada ya kichapo wikendi

adminleo