• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Kenya Simbas na Zambia zinafufua uhasama raga ya Victoria Cup

Kenya Simbas na Zambia zinafufua uhasama raga ya Victoria Cup

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya wanaume ya raga ya Kenya ya wachezaji 15 kila upande almaarufu Simbas itatafuta kuandikisha ushindi wake wa pili mfululizo dhidi ya Zambia itakapoalikwa uwanjani Diggers RC mjini Kitwe kwa mechi ya mashindano ya mataifa manne ya Victoria Cup, leo Jumamosi.

Simbas iliwasili nchini Zambia Alhamisi asubuhi na kufanya mazoezi uwanjani Kitwe baadaye siku hiyo.

Mabingwa wa Afrika mwaka 2011 na 2013 Kenya wamewahi kukutana na Zambia mara moja pekee katika historia yao.

Walipepeta Wazambia 33-10 katika mechi ya chungu cha pili kilichojumuisha pia Namibia katika zoni ya kusini ya Kombe la Afrika la mwaka 2004 jijini Nairobi.

Kenya ilikosa kufika fainali baada ya kubwagwa na Namibia 65-7 katika mechi ya chungu hiki kilichojumuisha timu tatu.

Tangu wakati huo, Kenya na Zambia hazijakutana tena katika raga ya wachezaji 15 kila upande, bali tu katika raga ya wachezaji saba kila upande.

Kenya, ambayo inashikilia nafasi ya 32 duniani kwa alama 52.25, itajiongezea alama chache sana ikipiga nambari 65 duniani Zambia. Hata hivyo, Simbas itarukwa na Colombia, Poland na Lithuania, ambazo zina alama 50.76, 50.59 na 49.45, ikipoteza.

Vijana wa kocha Paul Odera huenda pia watajipata pabaya zaidi kwenye viwango bora vya raga duniani wakipoteza halafu mmoja kati ya Uganda na Zimbabwe ishinde mechi nyingine ya mashindano haya jijini Kampala mnamo Julai 17.

Vikosi

Zambia (wenyeji) – Ali Bhika (nahodha), Berthlock Sikaona, Mphatso Hillary Mwashi, Kasonde Patson, Fine Chinkumbe (nahodha msaidizi), Jason Thole, Israel Kalumba, Laston Mukosa, Rodgers Mukupa, Edward Mumba (nahodha msaidizi), Sonny Nkole, Elisha Bwalya, Isaac Sakala, Brian Mbalwe, Gift Kabungo, John Kabwela, Ian Smith Mukupuka, Mike Masabo, Lawrence Nonde Kaushiku, Melvin Banda, Larry Kaushiku, Chisenga Jubilee na Pekah Phiri. Kocha – Lawrence Njovu (Zambia)

Kenya (wageni) – Simiyu Oscar, Francombe Toby, Thairu Melvin, Muniafu Simon, Onsando Malcolm, Amonde Andrew, Akuei Monate, Musonye Elkeans, Onsomu Samson, Kuka Charles, Odhiambo Billy, Mung’au Johnstone, Kilonzo Peter, Ojee Jacob, Odhiambo Anthony, Musila Griffin, Ouko Patrick, Lilako Curtis, Shem Joseph, Oloo Fidel, Wanjala Michael, Tendwa Charles na Njoroge Isaac. Kocha – Paul Odera (Kenya)

Ratiba ya Victoria Cup (2019)

Julai 13 – Uganda 5-16 Kenya (Elgon Cup & Victoria Cup mjini Kampala), Zimbabwe 39-10 Zambia (Victoria Cup mjini Harare);

Julai 27 – Zambia na Kenya (Victoria Cup mjini Kitwe), Uganda na Zimbabwe (Victoria Cup mjini Kampala);

Agosti 3 – Zimbabwe na Kenya (Victoria Cup nchini Zimbabwe);

Agosti 10 – Uganda na Zambia (Victoria Cup mjini Kampala);

Agosti 24 – Kenya na Zambia (Victoria Cup mjini Nairobi);

Septemba 21 – Kenya na Zimbabwe (Victoria Cup mjini Nairobi).

  • Tags

You can share this post!

Walichoandika baadhi ya watumiaji mitandao ya kijamii...

KILIMO: Manufaa ya mbegu za ndizi zilizoimarishwa...

adminleo