Kenya Simbas yaumwa na Cranes raga ya wanaume, Kenya Lionesses nayo yararua She Cranes raga ya wanawake Elgon Cup
Na GEOFFREY ANENE
KENYA Simbas imeanza kampeni yake ya kutetea ubingwa raga ya wachezaji 15 kila upande ya Kombe la Elgon kwa mguu mbaya baada ya timu hiyo ya wanaume kupoteza 13-16 katika mchezo wa Jumamosi uwanjani Mamboleo mjini Kisumu.
Timu ya wanawake ya Kenya nayo imejiweka katika nafasi nzuri ya kuhifadhi taji baada ya kulipua Uganda 42-13 katika mechi iliyotangulia kusakatwa uwanjani humu.
Simbas ya kocha Paul Odera ilijipata chini alama 0-11 baada ya Adrian Kasito kufunga mguso bila mkwaju. Aaron Ofoyrwoth aliimarisha uongozi huo kupita bao la alama tatu (drop goal) kabla ya kufanya mambo kuwa 11-0 alipopachika penalti.
Dominic Coulson alipunguza mwanya huo hadi 11-3 kupitia kwa penalti, lakini Uganda ilijibu kupitia mguso kutoka kwa Santos Senteza 16-3.
Kenya ilipata mguso wake wa kwanza na kufanya mambo kuwa 16-8 kupitia kwa Griffin Musila, lakini mkwaju wa Coulson uligonga mlingoti na kutoka nje.
Mguso mwingine kutoka kwa Geoffrey Okwach ulileta Kenya karibu na Uganda 16-13, huku mkwaju ukijaa nje. Ofoyrwoth aliibuka mchezaji bora wa mechi.
Vikosi
Kenya Simbas:
1. Sorano Oscar (KCB), 2. Francombe Toby (Nondies), 3. Odero Joseph (Kabras Sugar), 4. Muniafu Simon (Impala), 5. Silungi Emanuel (Homeboyz), 6. Akuei Monate (Nakuru), 7.Coulson Cameron (Durham University), 8. Musonye Elkeans (Impala Saracens, nahodha msaidizi), 9. Onsomu Samson (Impala Saracens), 10. Coulson Dominic (hana klabu), 11. Odhiambo Billy (Impala Saracens), 12. Okoth John (Nakuru), 13. Kilonzo Peter (KCB, nahodha), 14. Okwach Geoffrey (KCB), 15. Njoroge Isaac (KCB); Wachezaji wa akiba – 16. Musila Griffin (KCB), 17. Ouko Patrick (Homeboyz), 18. Oduor Ephraim (Kabras Sugar), 19. Onsando Malcolm (Harlequin), 20. Nyambua George (Kabras Sugar), 21. Wanjala Michael (KCB), 22. Kuka Charles (USIU), 23. Mutuku Jeff (Harlequin).
Uganda Cranes:
1. Santos Senteza, 2. Saul Kivumbi, 3. Asuman Mugerwa, 4. Collin Kimbowa, 5. Ronald Kanyanya, 6. Joseph Kagimu, 7. Charles Uhuru, 8. Robert Aziku, 9. Simon Olet, 10. Desire Ayera, 11. Brian Asaba, 12. Eliphaz Emong, 13. Byron Oketayot, 14. Aaron Ofoyrwoth, 15. Paul Epilo, 16. Robert Masendi, 17. Pius Ogena, 18. Ian Munyani, 19. Jordan Bongomin, 20. Paul Masendi, 21. Daudi Semwami, 22. Adrian Kasito, 23. Maxwell Ebonga.