• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Kenya yahimizwa kuiga mataifa ya Ulaya kukuza wanawake katika soka

Kenya yahimizwa kuiga mataifa ya Ulaya kukuza wanawake katika soka

NA TOTO AREGE akiwa Mjini Barcelona, Uhispania

MCHEZAJI wa zamani wa Harambee Starlets Jackline Juma anasema, Kenya inahitaji kuiga mataifa ya Ulaya, katika kukuza soka la wanawake nchini. 

Juma aliiongoza timu ya wasichana chini ya umri wa miaka 19 ya Talanta Hela hadi nafasi ya pili katika mashindano ya Kombe la Costa Daurada mjini Barcelona, ??Uhispania Alhamisi, wiki jana.

Kenya ilipoteza kwa mabao 2-0 katika fainali dhidi ya Sporting de Portugal ya Ureno baada ya mechi kuisha 1-1 katika muda wa kawaida.

Sasa ni dhahiri kwamba, soka ya wanawake inaendelea kukua.

Juma alielezea nguzo tatu muhimu ambazo ukuaji wa soka kwa wanawake nchini Kenya unapaswa kuzingatiwa.

“Napendekeza udhamini wa ligi ya wanawake ili kuongeza ushindani na kuvutia zaidi na ligi pia iwe na wadhamini kusaidia wanawake kifedha. Ligi ya vijana kuanzia ngazi za chini zitunzwe kwa umakini,” alisema Juma.

“Baada ya kambi ya Uhispania, tunahitaji kuendelea kuwafuatilia tukiwa nyumbani. Tunahitaji kucheza mechi za kirafiki na timu ambazo zimestawi kisoka. Mashindano ya Daurada yalikuwa mazuri ingawa tulipoteza kwenye penalti. Nimejifunza mengi ambayo pia nitawafunza makocha wenzangu nyumbani,”aliongeza Juma ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu ya wasichana chini ya miaka 20.


Kocha wa timu ya Talanta Hela ya wasichana ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 19 Jackline Juma, baada ya kuongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya pili katika michuano ya Kombe la Coasta Daurada nchini Uhuspania Machi 28, 2024 katika uwanja wa Academia ya Nastic mjini Taragona. PICHA|TOTO AREGE

Juma anaeleza changamoto zinazotokana na kufundisha wachezaji chipukizi.

“Kufundisha wachezaji wachanga ni changamoto. Wachezaji hawa wanatoka mazingira tufauti na lazima niwaelewe wote na kuwapa usawa,” aliongeza juma.

Mkufunzi huyo aliyeidhinishwa na leseni za CAF A, B, na C ana vyeti katika programu ya uhasibu ‘QuickBooks’, Uongozi, na Utawala katika soka ya wanawake chini ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Yeye pia ni mkufunzi wa timu ya Gor Mahia Queens ya ligi La Daraja la Kwanza.

Alikuwa mchezaji wa Mathare United Women, Old is Gold, na Makolanders aliistaafu soka mwaka 2016 baada ya miaka 20 ya kucheza soka.

Mchezo wa wanawake nchini Uhispania sasa umefikia viwango vya kimataifa. Mwaka jana,2023,  Uhispania ilishinda Kombe la Dunia nchini New Zealand na Australia.

Sergi Salvado ni mkufunzi wa utimamu wa mwili katika Nastic Soccer Academy (NSA) nchini Uhispania anasema,

“Mnamo Juni 2022, shirikisho la kandanda la Uhispania lilitangaza kwamba wachezaji wa kiume na wa kike watalipwa kwa usawa wanapowakilisha nchi yao. Makubaliano haya, yaliyochukua misimu mitano ijayo, yatahakikisha usawa katika usafiri, chakula na malazi kwa timu za taifa za Uhispania. Timu za wanawake zinatumia vifaa sawa na vya wanaume, jambo ambalo limechangia mafanikio yetu katika soka,” Salvado alisema.

Kwa mfano, mikoa ya Tarragona, Girona, Barcelona, na Lleida nchini Uhispania kila moja ina zaidi ya viwanja 100 vya mazoezi, na kila klabu ina timu ya wanawake.

Talanta Hela na timu ya wasichana na wavulana zinaendelea na kambi ya mazoezi na mechi za kirafiki Barcelona.

Wachezaji kama washambuliaji William Gitama, Hamisi Otieno na winga Jeremiah Bisau wamevutia vilabu vikubwa nchini Uhispania.

Talanta Hela na timu ya wasichana na wavulana wanaendelea na kambi ya mazoezi mjini Barcelona. Wachezaji kama washambuliaji William Gitama, Hamisi Otieno na winga Jeremiah Bisau wamevutia vilabu vikubwa nchini Uhispania.

“Mechi hizi za kirafiki hutumika kuonyesha talanta zetu. Kuna maskauti ambao baadhi yao hawajulikani na wanakuja kututazama kwani tunajituma kila siku ,” alisema beki Samuel Indonyi.

  • Tags

You can share this post!

Kinaya mafuriko yakitatiza jiji licha ya mikakati kuzuia...

Arushwa jela kwa kosa la wizi wa kimabavu

T L