• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 5:55 AM
Kenya yatangaza ubabe kwenye Riadha za Dunia Under-20 Finland

Kenya yatangaza ubabe kwenye Riadha za Dunia Under-20 Finland

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya Kenya inatarajiwa kupokelewa kishujaa itakaporejea nchini Julai 17 (2.00am) baada ya kuibuka mabingwa wa Riadha za Dunia za Under-20 nchini Finland hapo Julai 15, 2018.

Kenya ilizoa medali sita za dhahabu, nne za fedha na moja ta shaba na kumaliza utawala wa Marekani iliyokuwa imeshinda makala matatu mfululizo (mwaka 2012, 2014 na 2016).

Celliphine Chespol (mita 3,000 kuruka viunzi na maji), Beatrice Chebet (mita 5,000), Edward Zakayo (mita 5,000), Rhonex Kipruto (mita 10, 000), George Manangoi (mita 1,500) na Solomon Lekuta (mita 800) walizoa medali za dhahabu katika vitengo vyao.

Mabingwa wa mwaka 2000, 2006 na 2010 Kenya walipata nishani za fedha kupitia kwa Ngeno Kipngetich (mita 800), Stanley Waithaka (mita 5,000), Leonard Kipkemoi Bett (mita 3,000 kuruka viunzi na maji) na Miriam Cherop (mita 1,500).

Naye Justus Soget alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 1,500.

Laban Kiplangat (mita 400), Solomon Boit (mita 10, 000), Moitalel Mpoke Naadokila, James Mucheru (mita 400 kuruka viunzi), Philip Mwema (Kuruka hatua tatu), Dominic Ndigiti (matembezi ya mita 10, 000) na Mary Moraa (mita 400) waliambulia pakavu.

Wawakilishi wengine wa Kenya waliokamilisha mashindano hayo bila medali ni Jackline Wambui (mita 800), Lydia Jeruto (mita 800), Edina Jebitok (mita 1,500), Mercy Chepkurui (mita 3,000 kuruka viunzi na maji), Jemutai Yego, Mercy Kirarei (mita 3,000) na Hellen Lobun (mita 5,000).

Mataifa 158 yashiriki makala haya ya 17 mjini Tampere.

Msimamo wa medali duniani (10-bora):

Timu Dhahabu   Fedha        Shaba

1.Kenya        6       4       1       11

2.Jamaica     4       5       3       12

3.Marekani   3       7       7       17

4.Ethiopia     3       2       4       9

5.Uingereza  3       1       2       6

6.A.Kusini     3       0       1       4

7.Australia    2       3       0       5

8.Japan        2       2       2       6

9.Ujerumani  2       0       2       4

10.Mexico       2       0       0       2

Msimamo wa medali Afrika (duniani kwenye mabano):

1(1)Kenya        6       4       1       11

2(4)Ethiopia        3       2       4       9

3(6)A.Kusini        3       0       1       4

4(26)Uganda      0       2       0       2

  • Tags

You can share this post!

Kipa aomba msamaha kwa kukubali kulimwa mabao 5

Ratiba ya Prinsloo Sevens yatolewa

adminleo