• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
#KenyaVsGhana: Vikosi vyatajwa, nyasi kuumia Kasarani

#KenyaVsGhana: Vikosi vyatajwa, nyasi kuumia Kasarani

Na Geoffrey Anene

MAKOCHA Sebastien Migne (Kenya) na Kwesi Appiah (Ghana) wametaja vikosi vyao vya wachezaji wataoanza mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Afrika (AFCON) kati ya Harambee Stars na Black Stars uwanjani Kasarani jijini Nairobi, Jumamosi.

Mfungaji bora wa Kenya miaka ya hivi karibuni Michael Olunga, ambaye ni mali ya klabu ya Kashiwa Reysol nchini Japan, ataongoza mashambulizi ya Harambee Stars.

Kenya inahitaji ushindi pekee ili kufufua matumaini ya kunyakua mojawapo ya tiketi mbili zilizoko mezani kutoka kundi hili la F. Olunga atashirikiana na Ovella Ochieng’, ambaye amekuwa akitandaza soka ya kuvutia iliyomfanya anyakuliwe na klabu ya Vasalund nchini Uswidi miezi michache iliyopita. Kipa bora wa Kenya mwaka 2016 na 2017 Patrick Matasi, ambaye pia aliibuka kipa bora Kenya iliponyakua taji la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) Desemba mwaka 2017, ataanza michumani.

Macho yote katika kikosi cha Ghana yatakuwa kwa nyota wa zamani wa Chelsea, Christian Atsu, ambaye wakati huu ni mchezaji wa Newcastle United nchini Uingereza. Atsu hakuwa katika kikosi cha Ghana kilichobwaga Ethiopia 5-0 katika mechi ya ufunguzi mwaka 2017. Anafahamika kwa kasi na chenga za maudhi. Mvamizi matata wa Levante nchini Uhispania Raphael Dwamena, ambaye alifungia Ghana mabao mawili ikirarua Ethiopia, ataanza kwenye benchi.

Ghana inaongoza kundi hili kwa alama tatu kutokana na ushindi huo mkubwa dhidi ya Ethiopia. Inafuatiwa kwa tofauti ya magoli na Sierra Leone, ambayo ililemea Kenya 2-1 jijini Sierra Leone.

Kenya na Ethiopia hazina alama.

VIKOSI

Kenya

Wachezaji 11 wa kwanza – Patrick Matasi (kipa), Philemon Oieno, David Ochieng’, Musa Mohammed, Abud Omar, Dennis Odhiambo, Ismael Gonzalez, Ovella Ochieng’, Erick Ouma, Johanna Kubasu na Michael Olunga

Ghana

Wachezaji 11 wa kwanza – 1. Richard Ofori (kipa) 12. Andy Yiadom 4. Dan Opare 3. Nicholas Opoku 18. Daniel Amartey 6. Afriyie Acquah 8. Ebenezer Ofori 7. Christian Atsu 14. Edwin Gyasi 5. Thomas Partey 9. Majeed Waris;

Wachezaji wa akiba – Lawrence Ati, Harrison Afful, Kwadwo Asamoah, Isaac Sackey, William Owusu, Raphael Dwamena, Rashid Sumaila

  • Tags

You can share this post!

King’asti auza ubikira mtandaoni akidai hajapata...

Ratiba ya michuano ya ligi ya Super 8

adminleo