• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Kevin De Bruyne afikia rekodi ya Thierry Henry katika kuchangia idadi kubwa zaidi ya mabao EPL

Kevin De Bruyne afikia rekodi ya Thierry Henry katika kuchangia idadi kubwa zaidi ya mabao EPL

Na CHRIS ADUNGO

KIUNGO Kevin De Bruyne wa Manchester City amefikia rekodi ya aliyekuwa jagina wa soka kambini mwa Arsenal, Thierry Henry kwa kuchangia idadi nyingi zaidi ya mabao katika msimu mmoja wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

De Bruyne ambaye ni mzawa wa Ubelgiji, alichangia bao la 20 la msimu wa 2019-20 lililojazwa wavuni na kiungo Raheem Sterling katika ushindi wa 5-0 uliosajiliwa na Man-City dhidi ya Norwich City mnamo Julai 26, 2020 uwanjani Etihad.

Ufanisi huo ulimwezesha De Bruyne, 29, kumfikia Henry aliyechangia mabao 20 ya EPL akivalia jezi za Arsenal mnamo 2002-03.

“Ni fahari kwamba nimefikia rekodi hii. Sikuwahi kuamini kwamba nitafikia hapa nilipo na niwe hivi nilivyo. Natambua ukubwa wa mchango wa wanakikosi wenzangu kwa hatua hii muhimu. Tija zaidi ni kwamba nimeifikia rekodi ya Henry, mwanasoka ambaye nilikuwa nikimstahi sana udogoni,” akatanguliza.

“Jukumu langu ni kuchangia mabao uwanjani. Mara chache nikipata fursa za kufunga najaribu kufanya hivyo. Pongezi zaidi kwa wanasoka wa Man-City kwa kuwa rekodi hii isingekuja iwapo wasingepachika wavuni mipira kutokana na fursa nilizowaundia,” akasema nyota huyo wa zamani wa VfL Wolfsburg na Chelsea.

Hadi alipochangia mabao 20 katika msimu wa 2019-20, idadi kubwa zaidi ya magoli ambayo mwanasoka huyo alikuwa akijivunia kuchangia katika EPL ni 18 katika msimu wa 2016-17. Kwa sasa anajivunia kuchangia mabao 66 kutokana na mechi 154 za EPL.

De Bruyne anasalia katika nafasi ya 15 katika orodha ya wachangiaji bora zaidi wa mabao katika EPL tangu 1992. Orodha hiyo inaongozwa na nguli wa soka kambini mwa Manchester United, Ryan Giggs (162).

WACHANGIAJI BORA ZAIDI WA MABAO KATIKA MSIMU MMOJA WA EPL:

MCHEZAJI MSIMU IDADI YA MABAO

Kevin De Bruyne (Man-City) 2019-20 2-0

Thierry Henry (Arsenal) 2002-03 20

Mesut Ozil (Arsenal) 2015-16 19

Kevin De Bruyne (Man-City) 2016-17 18

Cesc Fabregas (Chelsea) 2014-15 18

Frank Lampard (Chelsea) 2004-05 18

Cesc Fabregas (Arsenal) 2007-08 17

Eric Cantona (Man-Utd) 1992-93 16

Kevin De Bruyne (Man-City) 2017-18 16

  • Tags

You can share this post!

Bunge la Zimbabwe lasitisha vikao

Pwani kuenda kortini

adminleo