Michezo

Kiatu cha Dhahabu: Nani atambwaga Harry Kane?

June 25th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na GEOFFREY ANENE

MUINGEREZA Harry Kane anaongoza vita vya kushinda Kiatu cha Dhahabu katika Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Mvamizi huyu wa Tottenham Hotspur amepachika mabao matano. Yuko bao moja mbele ya mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo (Ureno) na mvamizi wa Manchester United Romelu Lukaku (Ubelgiji).

Mrusi Denis Cheryshev kutoka klabu ya Villarreal na Mhispania Diego Costa, ambaye anasakata soka yake ya malipo Atletico Madrid, wameona lango mara tatu kila mmoja. Philippe Coutinho (Barcelona/Brazil), Artem Dzyuba (Arsenal Tula/Urusi), Eden Hazard (Chelsea/Ubelgiji), Mile Jedinak (Aston Villa/Australia), Luka Modric (Real Madrid/Croatia), Ahmed Musa (CSKA Moscow/Nigeria) na John Stones (Manchester City/Uingereza) wametikisa nyavu za wapinzani mara mbili kila mmoja.

Mfaransa Just Fontaine anashikilia rekodi ya mabao mengi katika makala moja ya Kombe la Dunia alipotikisa nyavu mara 13 mwaka 1958. Mchana-nyavu matata wa Argentina na Barcelona, Lionel Messi, ambaye alishinda taji la mchezaji bora mwaka 2014 nchini Brazil, bado hana bao nchini Urusi.

Mwaka       Mfungaji Bora

2014: James Rodriguez (Colombia) mabao 6

2010: Thomas Muller (Ujerumani) 5

2006: Miroslav Klose (Ujerumani) 5

2002: Ronaldo (Brazil) 8

1998: Davor Suker (Croatia) 6

1994: Histro Stoichkov (Bulgaria), Oleg Salenko (Urusi) 6

1990: Salvatore Schillachi (Italia) 6

1986: Gary Lineker (Uingereza) 6

1982: Paolo Rossi (Italia) 6

1978: Mario Kempes (Argentina) 6

1974: Gregorz Lato (Poland) 7

1970: Gerd Muller (Ujerumani) 10

1966: Eusebio (Ureno) 9

1962: Florian Albert (Hungary), Valentin Ivanov (Muungano wa Usovieti), Drazen Jerkovic (Yugoslavia), Leonel Sanchez (Chile), Vava (Brazil), Garrincha (Brazil) wote mabao 4

1958: Just Fontaine (Ufaransa) 13

1954: Sandor Kocsis (Hungary) 11

1950: Ademir (Brazil) 9

1938: Leonidas (Brazil) 8

1934: Oldrich Nejedly (Czechoslovakia), Edmund Conen (Ujerumani), Angelo Schiavio (Italia) wote mabao 4

1930: Guillermo Stabile (Argentina) 8