• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 5:07 PM
Kigogo Mascherano astaafu rasmi kwenye ulingo wa soka

Kigogo Mascherano astaafu rasmi kwenye ulingo wa soka

Na MASHIRIKA

KIUNGO wa zamani wa Barcelona na Liverpool, Javier Mascherano amestaafu rasmi kwenye ulingo wa soka.

Hadi alipoifikia hatua hiyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 alikuwa akichezea kikosi cha Estudiantes katika taifa la Argentina.

Katika enzi za ubora wake uwanjani, Mascherano alinyanyua mataji ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mara mbili na makombe matano ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga).

“Natangaza kwamba nastaafu rasmi kwenye soka ya kitaaluma hii leo. Nashukuru sana vinara wa kikosi cha Estudiantes kwa kunipa jukwaa la kusakata soka hadi nikafikia hatua ya kustaafu,” akasema.

Mascherano aliyeanza kutandaza soka akiwa mchezaji wa River Plate, anajivunia kuvalia jezi za timu ya taifa ya Argentina mara 147.

Aliwahi pia kuvalia jezi za klabu ya West Ham United nchini Uingereza kati ya 2006 na 2007 kabla ya kujiunga na Liverpool alikounga kikosi kilichopigwa na AC Milan kwenye fainali ya UEFA mnamo 2007.

Mascherano alichezea Barcelona kati ya 2010 na 2018 kabla ya kuyoyomea China kuwasakatia Hebei China Fortune.

  • Tags

You can share this post!

Kenya yateuliwa kupambana na New Zealand, Poland,...

MKU yapata ufadhili