• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 1:13 PM
Kikosi cha Tanzania chawekewa Sh80 milioni mezani wakikung’uta DR Congo

Kikosi cha Tanzania chawekewa Sh80 milioni mezani wakikung’uta DR Congo

Na SINDA MATIKO

BAADA ya kulazimishiwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Zambia, majirani Watanzania wengi walionyesha kuumizwa sana na timu yao ya Taifa Stars inayoiwakilisha Jumuiya ya Afrika Mashariki katika dimba la Bara Afrika AFCON kule Ivory Coast.

Taifa Stars walikuwa na fursa kibao za kuishinda mechi hiyo ya pili ya kundi F baada ya Chipolopolo kulishwa kadi nyekunde mapema mchezoni katika kipindi cha kwanza.

Hii ikiwa ni dakika 33 baada ya Simon Msuva kupokea pasi safi kutoka kwa kapteni wao Mbwana Samatta na kuwapachikia bao maridadi vijana wa mama Samia Suluhu Samia.

Hapa kila Mtanzania akaamini watoto wa mama watapata ushindi kiurahisi lakini Chipolopolo walikuwa na mpango kazi tofauti.
Dakika ya 88, Patrick Daka akapachia bao la uchungu kusawazisha na kuwavunja mionyo Tanzania.

“Leo imeuma zaidi asanteni vijana wetu Taifa Stars mmepambana haina kushika tamaa,” akaandika Waziri wa Michezo na Sanaa.

Ila mbunge wa Makete Festo Richard hakuficha kukeketwa kwake na kuwazomea.

“Watu wapo pungufu, una goli moja mchezo umeukamata. Kinachokushinda kuweka presha kupata goli la pili ni nini? Hesabu za Uchumi (Finacial Risk) zimetupita? Una elfu moja unatumia nguvu kubwa kulinda isizalishe? Uchumi wako utakuaje? Back pass dakika 45 for what? Kifupi mmetuumiza sana Watanzania,” Mbunge Richard akachefua.

Msanii Izzo Bizness naye akaishauri serikali kuachana kabisa kuigharamia Taifa Stars.

“Kama kuna uwekezaji wowote ambao serikali ilipanga kufanya mpira wa miguu nashauri hizo pesa zikatumike  kwenye kuongeza zahanati na mawdawa na huduma za maji safi kwa wananchi,” akatoa nasaha Bizness.

Matokeo hayo yalicha Taifa Stars ikivuta mkia kwenye kundi F inayoongozwa na Morocco kwa alama nne, DR Congo wakifuata na alama mbili sawia na Zambia katika nafasi ya tatu kutokana na tofauti ya magoli.

Sasa ili kufuzu kwa hatua ya muondoano ya 16 bora, Jumatano saa tano usiku Taifa Stars ni lazima isajili ushindi dhidi ya Mkongomani.

Ili kuwapa hamasa serikali ya mama Samia imewaahidi dola 500,000 (Sh81 milioni) wachezaji na benchi la ufundi ikiwa ni zawadi  endapo watafuzu hatua ya 16 bora kwa kuifunga DR Congo.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro amesema ahadi hiyo ya fedha imetolewa ili kuwaongezea hamasa kwa wachezaji.

  • Tags

You can share this post!

KWS yamwokoa mwanapundamilia akinyonya maziwa ya mzoga wa...

Mrembo wa kusaka mamilioni kwa mahindi aona dalili za ndoa...

T L