• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Kikosi cha voliboli All African Games chatajwa

Kikosi cha voliboli All African Games chatajwa

Na GEOFFREY ANENE

WENYEJI Kenya wamejawa na matumaini watafanya vyema kwenye mashindano ya voliboli ya wanaume ya Ukanda wa Tano hapo Juni 2-9, 2019 jijini Nairobi.

Akizungumza baada ya kutaja kikosi Jumatatu, kocha Moses Epoloto amesema, “Tumejiandaa vyema na tuko tayari kwa mashindano. Motisha yetu iko juu.”

Mataifa wanachama wa ukanda huu ni Kenya, Uganda, Rwanda, Misri, Tanzania, Sudan, Somalia, Ethiopia, Burundi, Sudan Kusini, Djibouti na Eritrea, ingawa ripoti zinasema nchi nane pekee zimeingia mchujo huu.

Mashindano haya yatatumiwa kuchagua timu itakayoshiriki michezo ya Bara Afrika ya All-African Games itakayofanyika jijini Rabat nchini Morocco kutoka Agosti 19-31, 2019.

Timu ya Kenya imekuwa ikifanya mazoezi yake katika ukumbi wa kimataifa wa Kasarani jijini Nairobi ambao pia utatumiwa kwa mashindano.

Baada ya kukosa tiketi ya kushiriki makala yaliyopita ya All-African Games nchini Congo Brazzaville mwaka 2015, Kenya itakuwa makini kupata tiketi nyumbani.

Matokeo mazuri ambayo Kenya imewahi kupata katika voliboli ya wanaume ya All-African Games ni medali ya shaba mwaka 2011 jijini Maputo nchini Msumbiji ilipopiga Rwanda 3-0 katika mechi ya kutafuta nambari tatu.

Wapinzani wakuu wa Kenya katika ukanda huu huwa Misri na Rwanda na haitarajiwi kuwa tofauti mwezi ujao. Uganda wamekuwa wakiimarika na hawawezi kupuuzwa. Epoloto anasaidiana na Paul Muthinja.

Kikosi cha Kenya:

Maseta – Brian Melly, Kelvin Kiposgei;

Washambuliaji wa pembeni kulia – Michael Chemos, Kelvin Omuse;

Washambuliaji wa pembeni kushoto – Jairus Kipkosgei (nahodha), Nicholas Matui, Sila Kipruto, Bonfentry Wekesa;

Wazuiaji wa kati – Rodgers Kipkirui, Simion Kipkorir, Linus Sang’, Sammy Ng’eny;

Malibero – Sam Juma, Noah Bett.

  • Tags

You can share this post!

Tunateseka, wakazi Lamu waitakata serikali kuwarudisha...

Jericho Allstars yateleza huku NYSA ikipiga hatua

adminleo