• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 8:55 PM
Kosgei na Obiri wang’aa mbio za San Silvestre, Uhispania

Kosgei na Obiri wang’aa mbio za San Silvestre, Uhispania

Na GEOFFREY ANENE

WAKENYA Brigid Kosgei na Hellen Obiri wamenyakua nafasi mbili za kwanza kwenye mbio za kilomita 10 za San Silvestre nchini Uhispania mnamo Desemba 31, 2018.

Kosgei, ambaye alishinda taji la Chicago Marathon mwezi Oktoba mwaka 2018, alinyakua ubingwa wake wa pili wa San Silvestre Vallecana baada ya mwaka 2016 kwa rekodi mpya ya dakika 29:54.

Alifuta rekodi ya Muethiopia Gelete Burka ya dakika 30:53 iliyowekwa mwaka 2012. Muethiopia Tirunesh Dibaba, ambaye alikuwa amepigiwa upatu kubeba taji, aliridhika katika nafasi ya tatu kwa dakika 30:40.

Nafasi tatu za kwanza za wanaume zilinyakuliwa na Mganda Jacob Kiplimo (dakika 26:41), Muethiopia Abadi Hadis (26:54) na Mganda Mashe Bushendich (27:24), mtawalia.

Kiplimo alivunja rekodi ya San Silvestre Vallecana ya dakika 26:54 ambayo mshikilizi wa sasa wa rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 42 Eliud Kipchoge aliweka akishinda taji la mwaka 2006.

Mbio hizi zilizovutia wakimbiaji 40, 000 zilianzia nje ya uwanja wa nyumbani wa Real Madrid Santiago Bernabeu na kukamilika ndani ya uwanja wa Rayo Vallecana viungani mwa jiji la Madrid.

  • Tags

You can share this post!

2018: Habari 10 zilizovutia wasomaji katika tovuti ya Taifa...

Mama ashinda mashindano bila kumpa fahali wake bangi

adminleo