KUFA KUPONA: Liverpool kukwaana na Atletico Madrid
Na MASHIRIKA
MERSEYSIDE, Uingereza
LIVERPOOL inajiadaa kutawazwa bingwa mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) lakini huenda ikashindwa kusonga mbele katika michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA) leo Jumatano usiku.
Hii ni baada ya vijana hao wa kocha Jurgen Klopp kulazwa 1-0 na Atletico Madrid katika mechi ya awali ya mkondo wa kwanza iliyochezewa Wanda Metropolitano, Uhispania.
Mbdele ya mashabiki wao wa nyumbani, Atletico walikuwa wamejipanga vyema kwa mchezo huo, baada ya kupewa nafasi ndogo ya kufuzu na mashabiki wengi. Walicheza vizuri na kushinda pambano hilo la nyumbani, lakini chochote chaweza kutokea sokani, wakati huu Liverpool wanatarajiwa kubadilisha mchezo wao na kucheza vizuri kuliko walivyocheza katika mkondo wa kwanza, ugenini.
Timu hizo zitakaporudiana leo usiku, Liverpool wanatakiwa wafunge mabao ya kutosha kuwawezesha kupata ushindi na kusonga mbele na kufufua matumaini ya kuhifadhi ubingwa wa taji hilo la bara.
Itakumbukwa kuwa walikuwa katika hali kama hii msimu uliopita, lakini wakabadilisha matokeo ya mkondo wa kwanza ya 3-0 dhidi ya Barcelona na kufuzu kwa fainali, kinyume cha matarajio ya wengi.
Iwapo wataibandua Atletico na kusonga mbele, bila shaka vigogo hao watakuwa miongoni mwa timu zitakazowekewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.
Jijini Paris, Ufaransa, mechi ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kati ya Paris Saint- Germain (PSG) na Borussia Dortmund itachezwa leo usiku bila uwepo wa mashabiki uwanjani kutokana na kusambaa kwa virusi vya Corona.
Maafisa wa usalama jijini hapa walisema hatua hiyo imechukuliwa kama tahadhari kwa mashabiki katika juhudi za taifa kupigana na maambukizi ya ugonjwa huo ulioanzia nchini China miezi mitatu iliyopita.
PSG ambao walishindwa 2-1 katika mkondo wa kwanza, watakuwa wenyeji wa pambano hili la marudiano katika uwanja wa Parc des Princes ulio na uwezo wa kubeba mashabiki 48,000.
Wasimamizi wa klabu hiyo wamesema watafanya wawezavyo kuhakikisha mechi hiyo imechezwa katika mazingara mazuri.
Kulingana na Shirika la Kimataifa la Afya (WHO), visa 1,116 vimeripotiwa nchini Ufaransa, huku ripoti hiyo ikisema kwamba mataifa yaliyoathirika zaidi ni China, Korea Kusini, Italia na Iran.
Kwingineko, AS Roma itavaana na Sevilla hapo Alhamisi katika mechi nyingine ya mkondo wa pili baada ya pambano la kwanza ugani Estadio Ramon Sanchez-Pizjuan,