• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Lloris akiri kuipa Liverpool ushindi

Lloris akiri kuipa Liverpool ushindi

Na CECIL ODONGO

MNYAKAJI wa Tottenham Hotspurs Hugo Lloris amekubali lawama kutokana na masihara aliyoyafanya langoni na kuiwezesha Liverpool kufunga bao dakika za mwisho kwenye mechi ya Ligi Kuu (EPL) Jumapili Machi 31 waliyoshindwa 2-1.

Hata hivyo, Lloris ameaihidi kurekebisha ulegevu huo uliowasaidia Liverpool kupata alama zote tatu ugani Anfield, Spurs itakapochuana na Crystal Palace kwenye mehi ya EPL Jumatano Aprili 3 ambayo pia itatumika kama jukwaa la kufungua uwanja wao wa kisasa wa White Hart Lane.

“Iwapo wewe ni mnyakaji una jukumu kubwa timuni kwa kuwa kosa dogo tu linatosha timu nzima kuzama . Hata hivyo nakubali kubeba lawama zote japo uzuri ni kwamba tuna mechi ndani ya siku tatu ambayo itakuwa jukwa bora la kurekebisha kosa hilo,” akasema Lloris.

“Nilijaribu kuushika mpira huo mara mbili lakini sikuweza kuufikia ndipo wakapata mwanya wa kufunga bao hilo. Ingawa tulikuwa na nafasi chache za kuweza kusawazisha bao hilo, hatukufanikiwa. Ni masikitiko makubwa,” akaongeza Lloris.

Spurs walionekana kupata uhai wakati wa mechi pale Lucas Moura alipofunga bao la kusawazisha lile la awali la Roberto Firmino . Ingawa hivyo Spurs walielekea kuchukua uongozi wa mechi kupitia Moussa Sissoko ila juhudi hizo zikazimwa na mabeki ngangari wa Liverpool.

Vijana wa Jurgen Klopp hatimaye walipata bao dakika za mwisho mwisho baada ya Lloris kushindwa kuuzuia mpira wa kichwa chake Mohamed Salah na beki Toby Alderweireld akaishia kujifunga mwenyewe.

You can share this post!

Mkataba wa Uhuru na Museveni utageuza Kenya mateka wa...

Ancelotti adai ataiondoa Arsenal Europa

adminleo