• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Maguire kusalia kapteni wa Manchester United licha ya kifungo

Maguire kusalia kapteni wa Manchester United licha ya kifungo

Na MASHIRIKA

BEKI Harry Maguire, 27, atasalia kuwa nahodha wa Manchester United licha ya kuhukumiwa kifungo ambacho kimeahirishwa kwa makosa kadhaa aliyoyafanya katika Kisiwa cha Syros, Ugiriki.

Nyota huyo wa timu ya taifa ya Uingereza alipatikana na hatia ya kushiriki fujo, kupinga kutiwa nguvuni na kujaribu kutoa hongo.

Hata hivyo, Maguire ambaye alitemwa kwenye timu ya taifa ya Uingereza amesisitiza kwamba hakuhusika katika tukio lolote la uvunjaji sheria na amekata rufaa dhidi ya hukumu aliyopokezwa.

“Atasalia kuwa nahodha wetu. Ameishughulikia kesi hiyo dhidi yake vilivyo na tutakuwa hapa kumsaidia,” akasema kocha Ole Gunnar Solskjaer.

Manchester watapimana ubabe na Aston Villa katika mechi ya kirafiki mnamo Septemba 12, 2020 kabla ya kufungua rasmi kampeni zao za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu dhidi ya Crystal Palace mnamo Septemba 19, 2020.

Hadi maamuzi ya kesi iliyokuwa ikimkabili Maguire yalipotolewa mnamo Agosti 25, nyota huyo alikuwa amejumuishwa na kocha Gareth Southgate kwenye kikosi cha Uingereza kilichovaana na Iceland na Denmark katika mechi za UEFA Nations League.

Southgate alisema kwamba kutemwa kwa Maguire kikosini mwake ni kwa minajili ya “maslahi ya pande zote husika”.

Kutokana na makosa aliyopatikana nayo katika eneo la Mykonos, Ugiriki, Maguire alipokezwa kifungo cha miezi 21 na siku 10 gerezani ila adhabu hiyo ikaahirishwa kwa miaka mitatu.

You can share this post!

Klabu anayochezea Malcolm Mamboleo yakamilisha ligi ya raga...

Arsenal wazamisha chombo cha Fulham katika EPL