• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:22 PM
MALI YA BORDEAUX: Koscielny aondoka Arsenal

MALI YA BORDEAUX: Koscielny aondoka Arsenal

Na MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

KLABU ya Arsenal imemuuza Laurent Koscielny aliyekuwa amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake na klabu hiyo ya ligi kuu ya Uingereza (EPL).

Mfaransa huyo amejiunga na klabu ya Bordeaux kwa Sh750 milioni.

Arsenal walitaka nyota huyo abakie klabuni lakini akafanya mgomo na kukataa kusafiri na timu kwenda kwenye ziara ya kujiandaa nchini Amerika.

Ikithibitisha habari hizo, Arsenal kupitia kwa mtandao wake rasmi iliksema: “Tumekubali ajiunge na Bordeaux baada ya kuafikia vyema kuhusu vigezo vya usajili. Tunamshukuru kwa mchango wake klabuni na tunamtakia kila la heri katika maisha yake ya baadaye.”

Koscielny alikataa mkataba mpya kuendelea kuchezea Arsenal, maarufu kama Gunners baada ya kuona kuwa vipengele vya mkataba huo vinavuruga mipango yake.

Hata hivyo, tayari Arsenal ilikuwa ikijiandaa kumuadhibu juu ya mgomo wake, kabla ya kumruhusu aendelee na mazoezi kwa ajili ya msimu mpya.

Koscienly kwa upande wake hakuwa na nia ya kubadili maamuzi yake ya kurejea nyumbani Ufaransa.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 33, alijiunga na Arsenal mwaka 2010 na kuichezea zaidi ya mechi 300.

Kumsajili beki mpya

Arsenal sasa inapigana vikali kumsajili beki mpya wa kati kabla ya dirisha la usajili nchini hapa kabla ya kufungwa leo Alhamisi.

Kwa sasa, miamba hao wako katika mazungmzo ya usajili kwa mlinzi Kieran Tierney wa Celtic mwenye umri wa miaka 22 na Carl Jenkinson wa Nottingham Forest mwenye umri wa miaka 27.

Kadhalika, klabu hii imekuwa na mipango ya kumuuza beki Shkodran Mustafi, lakini mpaka sasa hawajapokea ofa yoyote juu ya beki huyo Mjerumnai mwenye umri wa miaka 27.

  • Tags

You can share this post!

Atemwa na demu kwa kutomlipia karo

SHANGAZI AKUJIBU: Mpenzi hatulii mke wa kwanza kuhepa na...

adminleo