• Nairobi
  • Last Updated June 13th, 2024 10:55 AM
Man U wakanyaga shingo Aston Villa, huku Arsenal wakilipua West Ham bila huruma

Man U wakanyaga shingo Aston Villa, huku Arsenal wakilipua West Ham bila huruma

NA CHRIS ADUNGO

ARSENAL walipunguza pengo la alama kati yao na viongozi wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Liverpool, hadi pointi mbili baada ya kuponda West Ham United 6-0 ugani London Stadium, jana.

Na huko ugani Villa Park, miamba Manchester United waliangushia wenyeji Aston Villa kipigo cha 2-0, ambacho kimepunguza kasi ya vijana wa Unai Emery kukimbizana na taji, huku kikosi cha Erik Ten Hag kikiendeleza msururu wa matokeo bora.

Bao la kwanza la Man United lilifungwa na Rasmus Hojland kabla ya Douglas Luiz kusawazisha mapema katika kipindi cha pili. Hata hivyo, The Red Devils walijihakikisha alama zote tatu wakati Scott McTominay alipofunga bao la ushindi mchezo ukielekea kuisha.

Ushindi mnene wa Arsenal ulikuwa kwa kwanza kwao kusajili katika EPL ugenini tangu wakung’ute Aston Villa 7-1 mnamo Desemba 1935. Kilikuwa pia kichapo kinono zaidi kwa West Ham kupokea katika EPL nyumbani tangu wapepetwe 8-2 na Blackburn Rovers mnamo 1963-64.

Arsenal walijivunia uongozi wa 4-0 kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza kupitia magoli ya William Saliba, Gabriel Magalhaes, Leandro Trossard na Bukayo Saka aliyecheka na nyavu mara mbili. Goli jingine la Arsenal lilijazwa kimiani na nahodha wa zamani wa West Ham, Declan Rice.

Chini ya kocha Mikel Arteta, Arsenal sasa wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa jedwali la EPL kwa alama 52 sawa na mabingwa watetezi Manchester City ambao wana mchuano mmoja zaidi wa akiba.

  • Tags

You can share this post!

Madijei wanawake wanaowatoa wanaume jasho katika kucheza...

Njaa inavyoweka kina mama na wasichana kwenye hatari ya...

T L