• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Masaibu ya timu ya Taekwondo kutoka Maai Mahiu

Masaibu ya timu ya Taekwondo kutoka Maai Mahiu

NA RICHARD MAOSI

Karima Mixed Taekwondo ni kundi la wanamasumbwi na wapiganaji mahiri kutoka eneo la Maai Mahiu, wanaowakilisha Kenya kwenye jumuia ya mashindano Afrika Mashariki na kati.

Ni kikundi kilicho hasisiwa mnamo 2009 katika kaunti ya Nakuru ili kuwaleta pamoja wanafunzi wa shule za upili kote nchini,wenye vipaji katika ulingo wa michezo,ili waje kushindia taifa medali nyingi.

Mkufunzi wa Karima Mixed Timothy Mburu anasema eneo la Maai Mahiu limejaliwa vipaji vingi, isipokuwa serikali imewatelekeza wachezaji wengi kwa kukosa kuwapatia ufadhili ili wapate kuwa na hazina ya wanamichezo.

Anaona kuwa endapo vijana wengi watapata jukwaa la kutumia vipaji vyao ili kujiendeleza kimaisha ,wanaweza kuwa watu wa manufaa,aidha wataepuka swala la kutumia mihadarati na mimba za mapema.

Anasema kuwa kikosi chake kinajumuisha wachezaji wa jinsia ya kike na wale wa kiume, ambapo wao hufanya mazoezi yao kila siku za wiki kuanzia saa 4.00 -5.00 jioni.

Wakati wa likizo wao hujumuika kama desturi kujipiga msasa katika ukumbi wa Taekwondo unaopatikana mjini Maai Mahiu kilomita 42 kutoka jijini Nairobi.

Karima Mixed imekuwa ikishiriki katika michuano ya Interschools Competition inayohusisha shule zote za upili kutoka nchini Kenya ,ambapo walipata mafanikio makubwa sana mwaka wa 2018 walipofika kiwango cha kimataifa na kuwasilisha Kenya.

“Tuliwakilisha Kenya vyema kwenye mashindano ya Afrika Mashariki Kampala Uganda na hivi sasa tunajiandaa kushiriki katika michuano ya kitaifa itakayoandaliwa nchini Ujerumani,”mkufunzi Timothy Mburu akasema.

Miongoni mwa wanafunzi wake waliofana ni pamoja na Festus Waititu,Scolastica Wanjiru miongoni mwa wengine wengi.Festus alishindia Kenya nishani ya dhahabu kwa wachezaji chipukizi.

Timothy anasema kikosi chake kinachojumuisha wachezaji 50 kimefanikiwa kuwapatia wanafunzi mtazamo chanya kuhusu maisha,pia timu yake imewasaidia wanafunzi kudumisha nidhamu ya hali ya juu wakati wa mechi za nyumbani na zile za ugenini.

Alieleza kuwa shule ya Karima imekuwa ikiwawezesha wanafunzi ili waweze kupata mabuti,nauli za kushiriki mechi za ugenini,glavu na pesa za matumizi ya kawaida.

“Shule ya Karima pia imekuwa katika mstari wa mbele kulipia ada ya kutoa ukufunzi wa kitaaluma kwa kualika mabondia wanaotokea katika nyanja za kimataifa ili kuboresha kiwango na ujuzi wa wapiganaji,” akasema.

Licha ya kukosa ufadhili kutoka kwa serikali kuu na ile ya kaunti ya Nakuru wachezaji wengi hawajakata tamaa, wakiamini kuwa kipaji kinalipa muradi tu mchezaji awe na nia njia itapatikana.

Mwishoni mwa mwezi wa Oktoba Team Kenya inajiandaa kushiriki katika mashindano ya African Cup Team ambapo jumla ya wachezaji tatu kutoka Kenya zitawakilisha taifa.

Mashindano yenyewe yatakayofanyika katika mji mkuu wa Tanzania Dar -es-Salaam yanatarajiwa kuleta msisimko wa aina yake, ikizingatiwa timu nyingi kutoka Afrika zina uzowefu wa aina yake.

Mkufunzi Timothy anasema licha ya kutia juhudi nyingi kuwafikia wasimamizi wa michezo,idara husika imekuwa ikiwakwepa na kuwapatia ahadi za uongo ambazo mpaka sasa hazijawahi kuzaa matunda.

Hata hivyo anasema kuwa lengo lake kuu hivi sasa ni kuwasaidia wanafunzi wengi iwezekanavyo kujitosa katika ulingo huu wa kipekee usiokuwa na ufuasi mkubwa kama aina nyinginezo za michezo kama vile soka.

Anawashauri wazazi kuwashirikisha watoto wao katika sekta za spoti kwa sababu hii ni njia mojawapo ya kuleta mshikamano wa kitaifa bila kujali tabaka ,jinsia wala rangi ya mhusika.”Mambo yanayozingatiwa katika mchezo wa Taekwondo ni ya kimsingi kama vile tunafuata silabasi maalum kwa kuyafuata mafunzo ya kimsingi yanayochangia nidhamu ya hali ya juu,” akasema.

Aidha anasema anajaribu kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaelekezwa kwa njia inayofaa kwa sababu tunawekeza nidhamu ambapo mambo kama vile bidii,subira,ukakamavu,nidhamu na changamoto ni baadhi ya viungo muhimu vya kuzingatiwa ili kunogesha haiba ya mchezaji.

Mchezo wa Taekwondo ni wenye asili ya bara Asia huko Korea ambapo washiriki wengi walikuwa wakiutumia kama njia mojawapo ya kujikinga dhidi ya maadui hususan wakati wa kivita.

Lakini World Taekwondo Federation (WTF) iliunda Kenya Taekwondo Federation (KTF) ili wachezaji chipukizi wanaopatiakana mashinani waweze kufikiwa kwa urahisi.

Lakini taekwondo ya kimataifa ni bora kuliko ile ya kitaifa kwa sababu huzingatia mafunzo muhimu ya kumkuza mchezaji tangu akiwa mdogo hadi awe mahiri na kukomaa katika tasnia yenyewe.

“Vilabu vingi viliungana kote nchini na kutengeneza KTF ambayo inayumbayumba kutokana na ukosefu wa ufadhili mara kwa mara jambo linaloelekea kukwamisha shughui za mchezo huu,”akasema.

Makao makuu ya mchezo wa Taekwondo yanapatikana nchini Uhispania ambapo serikali ya Uhispania kupitia wahisani imekuwa ikiwanunuliwa baadhi ya wachezaji wa humu nchini sare rasmi za kufanyia mazoezi.

Lakini Timothy anasema kama wachezaji wengi watajihusisha na mchezo huu watapata tija kubwa,kwanza wataboresha afya yao kwa sababu ni njia moja ya kufanya mazoezi na pili watajiweka katika hatua nzuri ya kutengeneza ajira.

Anasema vijana wengi nchini wanafaa kujifua na kujitambua mapema kisha wawekeze uwezo wao wote katika shughuli zinazoboresha siha njema,maumbile,bidii na kazi.

Mbali na ukufunzi wa Taekwondo wanafunzi wa Karima wamekuwa wakifundishwa mbinu mbalimbali za kimaisha kama vile kutunza saa,ukulima na kupata ushauri nasaha.

Anaamini kuwa kikosi cha KenyTaekwondo kitakuja kuwasilisha taifa siku moja katika mashindano ya kimataifa bara ulaya, licha ya kudunishwa na wizara ya michezo.

You can share this post!

Kituo cha mafunzo ya soka Nakuru chalenga makuu

AKILIMALI: Arejea nchini kutoka China kufunza vijana jinsi...

adminleo