• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 12:38 PM
Kocha Gervais Hakizimana: Kielelezo cha urafiki wa kufa kuzikana kwa Kiptum

Kocha Gervais Hakizimana: Kielelezo cha urafiki wa kufa kuzikana kwa Kiptum

NA JOHN ASHIHUNDU

KOCHA Gervais Hakizimana alikuwa mkimbiaji mstaafu wa taifa la Rwanda aliyeshindia nchi yake mataji kadhaa katika mbio za masafa marefu, kabla ya baadaye kumuandaa marehemu Kelvin Kiptum aliyeaga dunia pamoja naye kwenye ajali ya barabarani Jumapili iliyopita.

Wengi walimtambua Hakizimana baada ya Kiptum kuvunja rekodi ya Dunia ya Marathon alipomaliza mbio hizo kwa muda wa 2:00:35 na kufuta rekodi ya awali ya muda wa 2:01:9 iliyokuwa ikishikiliwa na Eliud Kipchoge.

Hakizimana alizuru Kenya kwa mara mnamo 2006 akiwa na umri wa miaka 18 na kupiga kambi eneo la Kaptagat, Kaunti ya Uasin Gishu kwa mazoezi ya kujiandaa kwa mbio za Dunia za nyika zilizofanyika 2007 mjini Mombasa, alikoanzia taaluma yake ya kimataifa katika riadha.

Alimaliza katika nafasi ya 77 kwenye mbio hizo, kitengo cha wanaumme ambazo mshindi alikuwa Zersenay Tadese wa Eritrea, kabla ya baadaye kuwakilisha taifa lake la Rwanda katika mbio kilomita 10,000 jijini Algier Michezo ya Bara Afrika ilipofanyika nchini Algeria, akimaliza katika nafasi ya 17.

Hakizimana alikamilisha mwaka huo kwa kushiriki katika mbio za Half Marathon nchini Italia na kumaliza katika nafasi ya 38, huku Tadese akihifadhi ubingwa.

Hakizimana ambaye alikuwa amefanya Kaptagat kuwa nyumbani, alailazimika kurejea Rwanda kufuatia vita vya kabla na baadaye ya uchaguzi wa 2007 ambavyo viliathiri shugghuli katika sehemu nyingi, Rift Valley ikiwemo.

Aliendelea kushiriki katika mashindano mbali mbali mwaka uliofuata wa 2008, kabla ya kurejea kujaribu bahati katika mbio za Dunia za Great Britain ambapo hakufanikiwa kumaliza mbio hizo, pamoja na mbio za Half Marathon zilizofanyika Rio de Janeiro.

Hadi kifo chake kilichotokea Jumapili iliyopita, Hakizimana ndiye anayeshikilia rekodi ya taifa la Rwanda katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na vidimbwi vya maji. Vile vile alishiriki katika mbio za Great Britain Half Marathon mnamo 2009, na zile za nyika za Dunia zilizofanyika mnamo 2009, Jordan na 2011 kule Punta Umbria, Uhispania.

Hakizima alishiriki mbio za marathon kwa mara ya kwanza mnamo 2016, wakati wa London Marathon, alikojiondoa baada ya kukumbia kilomita 33 kutokana na jeraha, huku Eliud Kipchoge akimaliza kwa kuhifadhi taji hilo kwa mara ya pili.

Ingawa alihamia Ufaransa kwa masomo ya juu, mbali na kufanya kazi kwa miaka saba akiwa mkimbiaji, mara kwa mara alizuru Kenya kwa mazoezi.

Mrwanda huyo aliyekuwa na umri wa miaka 37 alizaliwa Wilaya ya Nyaruguru, Kusini mwa taifa hilo, lakini wakajuana na Kiptum mwaka 2009 akiwa kijana mdogo katika kijiji cha Chepsamo, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.

Kulingana na mjane Joan Chelimo, baadaye Kiptum aliungana na Hakizimana mazoezini na safari yake ikaanzia hapo.

  • Tags

You can share this post!

Pombe yaua tena Kirinyaga na kugeuza wawili kuwa vipofu

Ukiachwa achika, usiue mtu sababu ya mapenzi – Gavana...

T L