• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
Mooy ajiengua Brighton na kuhamia China kuchezea Shanghai SIPG

Mooy ajiengua Brighton na kuhamia China kuchezea Shanghai SIPG

Na CHRIS ADUNGO

KIUNGO mahiri mzawa wa Australia, Aaron Mooy, 29, ameyoyomea nchini China kuchezea Shanghai SIPG baada ya kuagana rasmi na kikosi cha Brighton nchini Uingereza.

Mooy alisajiliwa na Brighton almaarufu ‘Seagulls’ kwa mkopo kutoka Huddersfield Town mnamo Agosti 2019. Uhamisho huo ulirasimishwa kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

Akivalia jezi za Brighton, Mooy aliwajibishwa na kikosi hicho cha Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mara 32 msimu huu wa 2019-20 na akafunga mabao mawili.

“Mooy amekuwa mwanasoka stadi katika hiki kizima akiwa nasi. Uhamisho wake hadi China utamkuza zaidi kitaaluma,” akasema kocha wa Brighton, Graham Potter.

Shanghai SIPG kwa sasa wanashikilia nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu ya China (Chinese Super League).

You can share this post!

Gavana Mwangi wa Iria apigwa faini ya Sh500,000

Liverpool hawana haja na Messi – Klopp