• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Nairobi City Stars yazidi kutesa ligi ya NSL, Ushuru FC yazamishwa

Nairobi City Stars yazidi kutesa ligi ya NSL, Ushuru FC yazamishwa

Na JOHN KIMWERE

TIMU ya Nairobi City Stars iliendelea kukaa ngumu kwenye kampeni za kufukuzia taji la Supa Ligi ya Taifa (NSL) licha ya kutoka sare ya bao 1-1 na Mt Kenya United katika mechi iliyochezewa uwanjani Ruaraka, Nairobi.

Nazo Bidco United na Nairobi Stima kila moja ziliendelea kuwasha moto baada ya kutwaa ufanisi wa mabao 3-2 na 1-0 dhidi ya Vihiga Bullets na Modern Coast Rangers mtawalia huku Ushuru FC ikizamishwa kwa goli 1-0 na Vihiga United.

Ndoto ya City Stars kujiongezea pointi tatu ilikosa kutimia pale John Njoroge aliposawazishia Mt Kenya katika dakika ya 45 baada ya Jimmy Bagaya kuifungia dakika ya kwanza.

”Nashukuru vijana wangu walifanya kazi ya ziada ambapo bora alama moja kuliko kupoteza zote,” alisema kocha wa Mt Kenya, Thomas Okongo.

Nairobi Stima ilitia kapuni alama tatu muhimu kutokana na bao la usiku lililopachikwa kimiani na Joseph Shikokoti. Bidco ilibeba ufanisi huo kupitia Jacob Onyango alipojaza magoli mawili naye David Orem aliifungia goli moja.

Wafungaji wa Vihiga walikuwa Okello Baraza na Airo Godfrey.

Kwenye matokeo hayo, APs Bomet ilionekana imeanza kuamka ilipodunga St Josephs goli 1-0, FC Talanta ilishindwa mabao 2-0 na Migori Youth nayo Fortune Sacco ilipokezwa magoli 3-2 na Murang’a Seal.

Matokeo hayo yaliifanya City Stars kuendelea kukaa kileleni kwa alama 29, nne mbele ya Bidco.

  • Tags

You can share this post!

OBARA: Serikali ifunge madhehebu yanayoletea waumini maafa

IMF yapongeza vita dhidi ya ufisadi na mageuzi ya kiuchumi...

adminleo