Michezo

Orodha ya maafisa wa kaunti mbalimbali waliochaguliwa FKF

September 21st, 2020 Kusoma ni dakika: 2

Na GEOFFREY ANENE

Bodi ya Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) inatarajiwa juma hili kukutana na pande mbili zinazotofautiana kuhusu klabu zinazofaa kuchagua maafisa wa kaunti ya Garissa baada ya zoezi hilo kukosa kuendelea katika tawi hilo Jumamosi. Kaunti 20 kati ya 21 zilifanya uchaguzi wao Septemba 19.

“Garissa haikuchagua maafisa wake kwa sababu ya vuta-nikuvute kuhusu rejista ya klabu zinazofaa kushiriki zoezi hilo. Kuna mirengo miwili – moja unataka klabu 28 ziruhusiwe na mwingine unasema 18.

“Tulishindwa cha kufanya Jumamosi kwa sababu mrengo wa klabu 18 ulipata agizo kutoka kwa hakimu nao unaotaka klabu 28 zipige kura ukipata agizo kutoka kwa bodi ya rufaa inayotambuliwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA). Tutakutana na pande hizi kabla ya uchaguzi kufanyika,” alisema mwenyekiti wa uchaguzi wa FKF Kentice Tikolo.

Afisa huyo alisema uchaguzi wa mwakilishi wa vijana utarudiwa katika kaunti ya Vihiga. Kaunti zinatakiwa kufanya uchaguzi wao kufikia hapo Septemba 22 na kupisha shughuli la kusikiza na kuamua malalamishi kuhusu maafisa wapya wa kaunti kabla ya orodha rasmi ya washindi kuchapishwa Oktoba 1. Uchaguzi wa kitaifa ni Oktoba 17.

Hapo Jumamosi, kaunti za Mombasa, Kisumu na Laikipia pia zilikumbwa na matatizo. Masanduku ya kupigia kura yaliwasili Mombasa kuchelewa baada ya basi lilotumiwa kuharibika njiani. Kaunti ya Laikipia ilishuhudia mpiga kura mmoja akipigwa na wahuni na kupokonywa kitambulisho.

“Katika kaunti ya Kisumu, mgombea moja alifika katika kituo cha kupiga kura na kunyakua masanduku ya kupigia kura akitaka kuyaharibu. Kwa bahati nzuri, maafisa wa usalama waliingilia kati na kumtupa nje. Hizo ndizo changomoto tulizokumbana nazo Jumamosi,” alisema Tikolo.

Hii hapa orodha ya baadhi ya maafisa wa kaunti mbalimbali waliochaguliwa Jumamosi:

Kisumu – Dickson Oruko (mwenyekiti), Seth Oduor (katibu), Benta Owuor (mwakilishi wa wanawake), George Ouma (mweka hazina), Calvin Ogalo (mwakilishi wa vijana); Busia – Hillary Musundi (mwenyekiti), Reuben Olita (katibu), Bernard Onyango (mweka hazina), Josephine Oduori (mwakilishi wa wanawake), Martin Buluma (mwakilishi wa vijana); Nairobi East – Amos Otieno (mwenyekiti); Nairobi West – Caleb Malwenyi (mwenyekiti); Narok – Peter Karino (mwenyekiti), Elias Musunkuli (katibu), Paul Parmuat (mweka hazina), Ntirenye Dikirr (mwakilishi wa wanawake), Charles Ledama (mwakilishi wa vijana); Nyamira – Luthers Mokua (mwenyekiti); Mombasa – Alamin Abdalla (mwenyekiti); Kisii – Jezreel Mbegera (mwenyekiti), Evans Mageka (katibu); Baringo – Kenneth Ruto (mwenyekiti), Victor Situk (katibu), Willy Menego (mweka hazina), Jane Rotich (mwakilishi wa wanawake), Simon Arusei (mwakilishi wa vijana); Nakuru – Francis Oliele (mwenyekiti), Edmond Omungi (katibu), Peter Nderitu (mweka hazina), Dorcas Moraa (mwakilishi wa wanawake), James Angila (mwakilishi wa vijana); Kajiado – Alex Musekeri (mwenyekiti), Nathaniel Shukuru (katibu), Ishmael Nasoore (mweka hazina), Gladys Saunyi (mwakilishi wa wanawake), Hassan Abdirahman (mwakilkishi wa vijana); Nyandarua – Lucy Kageni Githinji (mwenyekiti), Joseph Thotho (katibu), Daniel Mwaura (mweka hazina), Eunice Wanjiru (mwakilishi wa wanawake), John Macharia (mwakilishi wa vijana); Nandi – Patrick Mutai (mwenyekiti), Joseph Wasike (katibu), Kennedy Kalya (mweka hazina), Tecla Lanet (mwakilishi wa wanawake), Alfred Kiprop (mwakilishi wa vijana); Kwale – Hamisi Mwakoja (mwenyekiti), Shilingi Omari (katibu), Bakari Hamisi (mweka hazina), Fatuma Mwinyi (mwakilishi wa wanawake), Alfanui Fadhili (mwakilishi wa vijana); Kakamega – Allan Muhando (mwenyekiti), Antony Okumu (katibu), Paul Andika (mweka hazina), Emily Muvango (mwakilishi wa wanawake), Enoch Lucheveleli (mwakilishi wa vijana).