• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
‘Pocket Rocket’ ajiuzulu mbio za New York City Half Marathon

‘Pocket Rocket’ ajiuzulu mbio za New York City Half Marathon

Vivian Cheruiyot. Picha/ Hisani

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Vivian Cheruiyot almaarufu Pocket Rocket alijiuzulu baada ya kutatizika kupumua katika mbio za New York City Half Marathon nchini Marekani mnamo Machi 18, 2018.

Vyombo vya habari nchini Marekani vimenukuu meneja wake Mike Skinner akisema bingwa huyu wa Olimpiki wa mbio za mita 5,000 ‘alitatizika kupumua kutokana na kibaridi kikali’ jijini New York.

Alifanyia mazoezi yake katika joto mjini Iten, kaunti ya Elgeyo-Marakwet, kabla ya kuelekea New York kwa makala hayo ya 13.

Cheruiyot alikuwa amekamilisha kilomita 16 katika mbio hizi za kilomita 21 kabla ya kujiuzulu.

Mabingwa Ben True (Marekani) na Buze Diriba (Ethiopia) walijishindia tuzo ya washindi ya Sh2, 024,990 kila mmoja.

True, ambaye alikamilisha mbio za kilomita 21 kwa mara yake ya kwanza kabisa, ni Muamerika wa kwanza kabisa mwanamume kushinda New York City Half Marathon.

Makala haya yalivutia wakimbiaji 22, 000, huku Wakenya wa kwanza kumaliza umbali huo wakiwa Wilson Chebet na Betsy Saina, ambao walikamilisha vitengo vya wanaume na wanawake katika nafasi za tisa na saba, mtawalia.

Wakenya Caroline Rotich, ambaye ni bingwa wa Boston Marathon mwaka 2015, na Grace Kahura, walimaliza katika nafasi za 10 na 14, mtawalia. Mkenya mwingine Stephen Sambu alikamilisha kitengo cha wanaume katika nafasi ya 14.

You can share this post!

Matumaini kwa Amerika kumaliza ukame wa miaka 32 bila taji...

Kikosi cha Chipu kwenye raga za Namibia chatajwa

adminleo