• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:50 AM
Rai aimarika zaidi viwango vya mbio za magari

Rai aimarika zaidi viwango vya mbio za magari

Na GEOFFREY ANENE

DEREVA Onkar Rai ameimarika zaidi kwenye jedwali la Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) mwaka 2019 baada ya kutawala duru ya KCB Meru Rally, wikendi.

Onkar, 31, ameruka kutoka nafasi ya nane hadi nambari tano. Kwa kushinda duru hiyo ya saba, Onkar alijiongezea alama 25 muhimu na kufikisha jumla ya alama 50.

Bingwa wa taifa mwaka 2008, 2013 na 2014 Baldev Chager anasalia kileleni kwa alama 141. Alikamilisha duru ya Meru katika nafasi ya tatu na kuvuna alama 18 muhimu. Yuko katika nafasi nzuri zaidi ya kumaliza ukame wa miaka minne bila taji la kitaifa.

Chager yuko alama 24 mbele ya mpinzani wake wa karibu Carl “Flash” Tundo aliyeridhika katika nafasi ya pili mjini Meru. Tundo ni bingwa wa Kenya mwaka 2007, 2009, 2012 na 2018.

Mfalme wa Afrika mwaka 2017, 2018 na 2019 Manvir Baryan anasalia katika nafasi ya tatu kwa alama 91. Alipata ajali katika Meru Rally.

Msimamo wa Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) baada ya KCB Meru Rally (nane-bora): Baldev Chager (pointi 141), Carl “Flash” Tundo (117), Manvir Baryan (91), Tejveer Rai (63), Onkar Rai (50), Ian Duncan (38), Amar Haq (33), Izhar Mirza (33).

  • Tags

You can share this post!

Kipkorir bingwa wa Athens Marathon

Mpasuko kisiasa ulichangia Uhuru kufuta ziara ya...

adminleo