Raphael Varane kupigwa bei ya jioni na Man United
NA CECIL ODONGO
MFARANSA Raphael Varane (pichani) anaongoza orodha ya mastaa wanaotarajiwa kuondoka Manchester United mwisho wa msimu huu.
Varane, 30, amepoteza makali aliyokuwa nayo Real Madrid akiwasaidia kuibuka mabingwa wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mara tatu mfululizo kabla yake kuhamia Old Trafford mnamo 2021.
Akiwa mmoja wa wachezaji wanaokula mshahara mnono Old Trafford (Sh55.4 milioni kila wiki), Man-United wako tayari kumuuza mwisho wa msimu huu ili wasibaki mikono mitupu kandarasi yake itakapokatika Juni 2025.
Msimu mwingine wa United wa masikitiko unaelekea kufika ukingoni bila dalili kuwa watakuwa wagombea halisi wa taji.
Matumaini ya kuingia Klabu Bingwa Ulaya yanaonekana ni ndoto tu.
Hata Ligi ya Uropa bado hakuna hakikisho nambari sita United watashiriki msimu ujao kwani vita vya kufuzu vingali wazi kwa karibu timu tano.
Si mara ya kwanza Mfaransa Varane,30, amehusishwa na uhamisho.
Bingwa huyo wa Kombe la Dunia 2018 aliyejiunga na United mwaka 2021, alisaidia timu hiyo kushinda Kombe la Carabao msimu 2022-2023, lakini majeraha yameathiri mchango wake.
Akiwa mmoja wa wachezaji wanaokula mshahara mkubwa Old Trafford (Sh55.4 milioni kila wiki), United wanaaminika wako tayari kumuuza mwisho wa msimu huu ili wasitoke mikono mitupu kandarasi itakapokatika Juni 2025.