• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 9:48 PM
Sare yavuruga mipango ya Jericho All Stars

Sare yavuruga mipango ya Jericho All Stars

Na JOHN ASHIHUNDU

Juhudi za Jericho All Stars kupanua mwanya katika uongozi wa ligi kuu ya Super 8 ziliambulia patupu baada ya kugana 3-3 na vigogo wa Dagoretti Former Players FC.

Mechi hiyo ilichezewa ugani Camp Toyoyo mbele ya mashabiki wengi waliomiminika uwanjani humo kushuhudia mastaa kadhaa wa Dagoretti ambao walichezea timu kubwa nchini.

Mapema uwanjani humo, Lebanon FC walipoteza nafasi nyingi kabla ya kulasimika kutoka sare 1-1 na Makadara Junior League. Eugene Oduor aliwafungia bao la kusawazisha dakika ya 70 kutokana na mkwaju wa penalti kuvuruga matumaini ya makadara waliotangullia kuona lango kupitia kwa bao la Marvin Wachai.

Ushindi katika mechi hiyo ungeiwezesha Jericho kuongoza msimamo wa ligi hiyo ya timu 16 kwa tofauti ya pointi saba.

Nahodha, Kelvin Ndungu aliifungia Jericho bao la kwanza dakika ya 31, na kuifanya timu yake kuongoza kwa bao hilop kufikia wakati wa mapumziko.

Muda mfupi baada ya muda huo kumalizika, Jericho walijipatia bao la pili kupitai kwa Bundu Engo kabla ya Steve Opuku kuongeza la tatu.

Huku wakitarajia kuibuka na ushindi wa 3-0, Maloba aliwafungia Dagoretti bao la kwanza dakika ya 72 kabla ya kuongeza la pili dakika ya 80.

Makosa ya mabeki wa Jericho yalimwezesha Ibrahim Kiranga kusawazisha mambo dakika ya 85.

Pointi hiyo moja imewafanya Dagoretti kubakia katika nafasi ya tisa kutokana na pointi 10.

Matokeo ya mechi za Super 8 kwa jumla yalikuwa: Jericho All Stars 3-3 Dagoreti Former Players FC; Makadara Junior League SA 1-1 Lebanon FC; Mathare Flames 1-1 Team Umeme; Meltah Kabiria FC 4-2 Metro Sports FC; Rongai All Stars 3-1 NYSA; TUK 1-1 Githurai All Stars.

You can share this post!

Huenda watumishi wa Ruto wakatupwa jela kwa wizi wa mayai

Ushindi kwa Butterfly, Tandaza yala sare

adminleo