Senegal katika Kundi C yataja kikosi chake tayari kwa AFCON
Na GEOFFREY ANENE
SENEGAL ni timu ya hivi punde kutoka Kundi C kutangaza kikosi chake cha Kombe la Bara (AFCON) baada ya Kenya na Algeria kufichua vikosi vyao Mei 30, 2019.
Wakali Sadio Mane (Liverpool, Uingereza), Kalidou Koulibaly (Naples, Italia), Idrissa Gana Gueye (Everton, Uingereza), Cheikhou Kouyate (Crystal Palace, Uingereza) na Keita Balde (Lazio, Italia) ni baadhi ya majina makubwa katika kikosi cha Lions of Teranga cha wachezaji 25 alichotaja Kocha Aliou Cisse hapo Mei 31.
Senegal itajipima nguvu dhidi ya Nigeria hapo Juni 16 kabla ya kufungua kampeni yake dhidi ya Tanzania hapo Juni 23.
Sebastien Migne, ambaye anonoa Harambee Stars ya Kenya, alijumuisha wachezaji matata Victor Wanyama (Tottenham Hotspur, Uingereza), Michael Olunga (Kashiwa Reysol, Japan), Ayub Timbe (Beijing Rehne, Uchina) na Francis Kahata (Gor Mahia) katika kikosi chake jijini Nairobi. Migne na vijana wake walitoka jijini Nairobi saa mbili na nusu asubuhi Ijumaa kuelekea jijini Paris nchini Ufaransa kwa kambi ya siku 19.
Kenya, ambayo inarejea katika AFCON tangu mwaka 2004, itapimana nguvu dhidi ya Madagascar mnamo Juni 7 jijini Paris na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jijini Madrid nchini Uhispania mnamo Juni 15 kabla ya kufunga safari ya Misri hapo Juni 19.
Naye kocha Djamel Belmadi wa timu ya Algeria anajivunia silaha hatari Sofiane Feghouli (Galatasary, Uturuki), Riyad Mahrez (Manchester City, Uingereza), Islam Slimani (Fenerbahce, Uturuki) na Yacine Brahimi (Porto, Ureno).
Desert Warriors itapiga kambi nchini Qatar mnamo Juni 8 na kujipima nguvu dhidi ya Burundi (Juni 11) na Mali (Juni 16) kabla ya kuelekea Misri.
Huku hayo yakijiri, majirani wa Kenya, Tanzania, ambao bado hawajataja kikosi chao, wanasemekana wanatatizika kifedha.
Gazeti la The Citizen limeripoti kwamba Taifa Stars inahitaji Sh2.3 bilioni za nchi hiyo kujiandaa kwa kurejea katika AFCON tangu mwaka 1980 mwezi ujao.
Gazeti la THISDAY nalo limesema Ijumaa kwamba Tanzania ya kocha Emmanuel Amuneke haitakuwa nchini Misri kujaza tu orodha ya washiriki 24 watakaokusanyika humo.
Tanzania, ambayo nyota wake ni Mbwana Samatta anayacheza nchini Ubelgiji, itasakata mechi za kirafiki dhidi ya Misri na Zimbabwe kabla ya kuanza kampeni yake ya AFCON.
Kenya itaanza kampeni yake ya Kombe la Afrika dhidi ya Algeria mnamo Juni 23. Mechi zote za kundi hili zitachezewa uwanjani 30 June jijini Cairo.
Vikosi vya Kundi B:
Kenya
Makipa – Patrick Matasi (St Georges, Ethiopia), John Oyemba (Kariobangi Sharks), Farouk Shikalo (Bandari);
Mabeki – Abud Omar (Sepsi Sf. Gheorghe, Romania), Joash Onyango (Gor Mahia), Joseph Okumu (Real Monarchs, Marekani), Musa Mohammed (Nkana, Zambia), David Owino (Zesco United, Zambia), Bernard Ochieng (Vihiga United), Brian Mandela (Maritzburg, Afrika Kusini), Philemon Otieno (Gor Mahia), Erick Ouma (Vasalund, Uswidi);
Viungo – Victor Wanyama (Tottenham Hotspur, Uingereza), Anthony Akumu (Zesco United, Zambia), Ismael Gonzalez (Las Palmas, Uhispania), Ayub Timbe (Beijing Renhe, Uchina), Francis Kahata (Gor Mahia), Ovella Ochieng (Vasalund, Uswidi), Dennis Odhiambo (Sofapaka), Eric Johanna (Brommapojkarna, Uswidi), Paul Were (AFC Leopards), Cliffton Miheso (Olimpico Montijo, Ureno), Johanna Omollo (Cercle Brugge, Ubelgiji);
Washambuliaji – John Avire (Sofapaka), Masoud Juma (hana klabu), Christopher Mbamba (Oddevold, Uswidi) na Michael Olunga (Kashiwa Reysol, Japan)
Senegal
Makipa – Abdoulaye Diallo (Rennes, Ufaransa), Alfred Gomis (SPAL, Italia), Edouard Mendy (Reims, Ufaransa);
Mabeki – Salif Sane (Schalke 04, Ujerumani), Kalidou Koulibaly (Naples, Italia), Pope Abou Cisse (Olympiacos, Ugiriki), Lamine Gassama (Goztepe, Uturuki), Moussa Wague (Barcelona, Uhispania), Youssouf Sabaly (Bordeaux, Ufaransa), Saliou Ciss (Valenciennes, Ufaransa);
Viungo – Idrissa Gana Gueye (Everton, Uingereza), Alfred Ndiaye (Malaga, Uhispania), Badou Ndiaye (Galatasaray, Uturuki), Krepin Diatta (Brugge, Ubelgiji), Cheikhou Kouyate (Crystal Palace, Uingereza), Sada Thioub ( Nimes, Ufaransa), Sidy Sarr (Lorient, Ufaransa), Henri Saivet (Bursaspor, Uturuki);
Washambuliaji – Keita Balde (Lazio, Italia), Sadio Mane (Liverpool, Uingereza), Moussa Konate (Amiens, Ufaransa), Ismaila Sarr (Rennes, Ufaransa), Mbaye Diagne (Galatasaray, Uturuki), Mbaye Niang (Rennes, Uturuki), Santy Ngom (Nancy, Ufaransa)
Algeria
Makipa – Rais M’Bolhi (El Etifaq, Saudi Arabia), Azzedine Doukha (Al Raed, Saudi Arabia), Alexandre Oukidja (Metz, Ufaransa);
Mabeki – Aissa Mandi (Real Betis, Uhispania), Mehdi Zeffane (Rennes, Ufaransa), Ramy Bensebaini (Rennes, Ufaransa), Rafik Halliche (Moreirense, Ureno), Mehdi Tahrat (Lens, Ufaransa), Djamel Benlamri (Al Shabab, Saudi Arabia), Youcef Atal (Nice, Ufaransa), Mohamed Fares (SPAL, Italia);
Viungo – Haris Belkebla (Brest, Ufaransa), Ismail Bennacer (Empoli, Italia), Mehdi Abeid (Dijon, Ufaransa), Sofiane Feghouli (Galatasary, Uturuki), Adlene Guedioura (Nottingham Forest, Uingereza), Hicham Boudaoui (Paradou, Algeria);
Washambuliaji – Adam Ounas (Naples, Italia), Riyad Mahrez (Manchester City, Uingereza), Islam Slimani (Fenerbahce, Uturuki), Yacine Brahimi (Porto, Ureno), Baghdad Bounedjah (Al Sadd, Qatar), Youcef Belaili (Esperance, Tunisia)