• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Starlets wana matumaini kwamba mara hii watazima Waghana

Starlets wana matumaini kwamba mara hii watazima Waghana

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya soka ya wanawake ya Kenya almaarufu Harambee Starlets imejawa na matumaini kuwa itafanya vyema dhidi ya Ghana katika mechi ya raundi ya tatu ya kufuzu kushiriki michezo ya Olimpiki mwaka 2020.

Starlets ya kocha David Ouma ilikamilisha mazoezi yake jana uwanjani Camp Toyoyo jijini Nairobi.

Iiratibiwa kusafiri saa kumi na moja alfajiri leo Jumanne.

Ouma, ambaye alitarajiwa kuchuja wachezaji watatu jana jioni kutoka kikosi cha wachezaji 23 aliokuwa nao kambini, alisema wamekuwa na maandalizi mema na kuongeza kuwa watajaribu kadri ya uwezo wao kudhibiti Black Queens jijini Accra, Oktoba 4.

“Tumekuwa na wiki mbili za mazoezi mema. Tunafahamu Ghana ni timu nzuri, lakini tutajaribu kuwadhibiti na hata kutafuta ushindi ugenini,” alisema Ouma.

Naye beki Dorcas Shikobe, ambaye ni nahodha, alisema, “Motisha yetu iko juu. Mbinu yetu ya kwanza katika mechi hiyo ya mkondo wa kwanza ni kuepuka kufungwa bao kwa kulinda ngome yetu vyema. Itakuwa muhimu pia tukipata bao la ugenini. Baada ya kupiga sare dhidi yao mjini Machakos mwaka uliopita, naamini Ghana ni timu tunayoweza kupiga.”

Mshambuliaji matata Mwanahalima Adam, ambaye alifunga mabao mawili Kenya ikibandua nje Malawi kwa jumla ya mabao 5-3 katika raundi ya pili Septemba 1, alikiri Ghana si timu rahisi.

  • Tags

You can share this post!

SHANGAZI AKUJIBU: Nimeacha mume wangu, mwalimu sasa anifuata

Kimanzi ataja vifaa 23 vya kukabili Msumbiji kirafiki

adminleo