• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 5:50 AM
Tanzania yatupwa nje ya Afcon awamu ya makundi

Tanzania yatupwa nje ya Afcon awamu ya makundi

NA LABAAN SHABAAN

TIMU ya kandanda ya Tanzania, Taifa Stars, imebanduliwa nje ya michuano ya Kombe la Afrika (Afcon 2023) baada ya kutoka sare tasa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Tanzania ikikata tiketi ya ndege kurudi Dar es Salaam, DRC imepata tiketi ya mkondo wa muondoano ikiwa na alama tatu na itakuwa na kibarua dhidi ya Misri mnamo Januari 28, 2024.

Pointi moja ilitosha kwa DRC kumaliza nafasi ya pili kundini F nyuma ya Morocco walioibuka kidedea kwa kuipiga kumbo Zambia 1-0.

Morocco watakabana koo na Afrika Kusini mnamo Janauri 30, 2024, katika mkondo huo wa kufa kupona.

Matokeo ya mechi za Kundi F yalisaidia wenyeji Cote d’Ivoire kuvaa daluga na sare tena kurejea ugani mkondo wa mtoano baada ya kuhisi wameaga mashindano wakiwa wenyeji.

Ivory Coast watapimana nguvu na mabingwa watetezi Senegal katika mkutano wa nani mkali mnamo Januari 29, 2024.

Michuano ya Afcon itachukua mapumziko ya siku mbili na kuendelea tena Januari 27, 2024, wakati pazia litafunguliwa kwa mchuano kati ya Super Eagles ya Nigeria na Cameroon.

Timu ambazo zilipata nafasi nne zilizotengewa mataifa washinde bora ni Cote d’Ivoire, Namibia, Mauritania, na Guinea.

  • Tags

You can share this post!

Saudi Arabia kufungua duka la pombe kwa mabalozi

Mr Seed akomoana na mkewe mtandaoni kwa kusema ‘mwanamume...

T L