TP Mazembe wainyeshea Atlabara 6-1 Kagame Cup
Na GEOFFREY ANENE
MABINGWA mara tano wa Klabu Bingwa Afrika, TP Mazembe walifundisha Atlabara kutoka Sudan Kusini jinsi ya kusakata soka baada ya kuwanyuka 6-1 katika mechi yao ya mwisho ya Kundi A kwenye mashindano ya Cecafa Kagame Cup nchini Rwanda, Jumamosi.
Mazembe, ambao wamealikwa kushiriki mashindano haya ya Afrika Mashariki na Kati, wamepata mabao yao kupitia kwa mshambuliaji Jackson Muleka dakika ya tatu na 52, kiungo Christian Kouame (15), beki Glody Likonza (46) na nahodha Rainfold Kalaba (65 na 88).
Ushindi huu mkubwa kabisa katika makala haya kufikia sasa, umehakikishia Mazembe tiketi ya kushiriki robo-fainali kama mshindi wa kundi na kuondoa Atlabara mashindanoni.
Waliokuwa viongozi wa kundi hili Rayon Sport (Rwanda) walichabangwa 1-0 na KMC (Tanzania) na kumaliza katika nafasi ya pili kwa tofauti ya ubora wa magoli. Wote wana alama sita. Rayon ilikanyaga Mazembe 1-0 katika mechi ya ufunguzi kabla ya kulima Atlabara 2-0 na kuingia robo-fainali.
Kenya imesalia na mwakilishi mmoja katika mashindano haya ambaye ni Gor Mahia. Gor itapepetana na KMKM kutoka Zanzibar katika mechi yake ya mwisho ya Kundi D leo Jumapili.
Ilijikatia tiketi ya robo-fainali baada ya kuzaba AS Maniema kutoka DR Congo 2-1 na AS Ports kutoka Djibouti 2-0 katika mechi zake zilizopita.
Bandari FC iliaga mashindano baada ya kupiga sare tatu dhidi ya Waganda KCCA (1-1), Mukura Victory kutoka Rwanda (2-2) na mabingwa watetezi Azam kutoka Tanzania (0-0).
Matokeo:
Julai 13
Atlabara 1-6 TP Mazembe – Kundi A
Rayon Sports 0-1 KMC – Kundi A
Julai 12
Azam 0-0 Bandari – Kundi B
KCCA 2-1 Mukura Victory – Kundi B
Julai 11
Proline 1-2 Green Eagles – Kundi C
APR 4-0 Heegan – Kundi C
Julai 10
AS Ports 0-2 Gor Mahia – Kundi D
KMKM 0-2 AS Maniema – Kundi D
Proline FC 1-2 Green Eagles FC – Kundi C
APR FC 4-0 Heegan FC – Kundi C
Julai 9
Bandari 2-2 Mukura Victory – Kundi B
KCCA 1-0 Azam – Kundi B
KMC 0-1 TP Mazembe – Kundi A
Atlabara 0-2 Rayon Sports – Kundi A
Julai 8
Proline 2-0 Heegan – Kundi C
AS Ports 2-0 KMKM – Kundi D
Gor Mahia 2-1 AS Maniema – Kundi D
Green Eagles 0-1 APR – Kundi C
Julai 7
Bandari 1-1 KCCA – Kundi B
KMC 1-1 Atlabara – Kundi A
Azam 1-0 Mukura Victory – Kundi B
Rayon Sport 1-0 TP Mazembe – Kundi A
Julai 6
Heegan 0-2 Green Eagles – Kundi C
APR 1-0 Proline – Kundi C