• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
Trippier kutumikia marufuku ya wiki 10 kwa kukiuka kanuni za kamari

Trippier kutumikia marufuku ya wiki 10 kwa kukiuka kanuni za kamari

MASHIRIKA na CHRIS ADUNGO 

DIFENDA wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Uingereza, Kieran Trippier amepigwa marufuku ya wiki 10 na kutozwa faini ya Sh9.8 milioni baada ya Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) kumpata na hatia ya kukiuka kanuni zinazodhibiti mchezo wa kamari.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 alikana madai saba ya kukiuka kanuni za mchezo huo wa bahati nasibu japo madai manne yaliyotolewa dhidi yake yalithibitishwa wakati wa kusikilizwa kwa kesi.

Trippier alikiuka kanuni za mchezo wa kamari mnamo Julai 2019 huo ndio wakati alipojiunga rasmi na Atletico kutoka Tottenham Hotspur.

Marufuku ambayo Trippier amepokezwa yanaanza kutekelezwa mara moja na hatatakiwa sasa kujihusisha na masuala yoyote ya soka kwa kipindi cha siku 70 zijazo.

Ina maana kwamba Trippier atakosa mechi 12 zijazo zitakazopigwa na Atletico ambao ni viongozi wa Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) ikiwemo mechi ya mkondo wa kwanza wa hatua ya 16-bora kwenye Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) dhidi ya Chelsea mnamo Februari 23, 2020.

Hata hivyo, nyota huyo atarejea ugani kwa minajili ya gozi kali la La Liga litakalowakutanisha Atletico na Real Madrid mnamo Machi 7, 2021.

  • Tags

You can share this post!

AKILIMALI: Hela anazorina kuuza dania, mbegu zake zilifanya...

Ruto akutana na Feisal baada ya kushinda kiti cha Msambweni