• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 4:26 PM
Uefa kudumisha sheria ya kuchezeshwa kwa wanasoka watano wa akiba

Uefa kudumisha sheria ya kuchezeshwa kwa wanasoka watano wa akiba

Na MASHIRIKA

VIKOSI vitakubaliwa kuchezesha wanasoka watano wa akiba katika mechi za Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) na Europa League hadi mwishoni mwa msimu wa 2020-21.

Sheria hiyo ilipendekezwa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa sababu ya mrundiko wa mechi uliochangiwa na janga la corona kuanzia Juni 2020.

Mnamo Agosti, klabu za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) zilisisitiza kwamba zingekumbatia mabadiliko hayo kwa madai kwamba yangenufaisha zaidi vikoi vikuu vinavyojivunia idadi kubwa ya wanasoka wa haiba hata katika orodha ya wachezaji wa akiba.

Hata hivyo, Rais wa Shirikisho la Soka la bara Ulaya (Uefa), Aleksander Ceferin amesema kwamba jumla ya wanasoka watano wa akiba watakubaliwa kucheza katika michuano ya UEFA, Uefa Nations League na Europa League.

Hata hivyo, wadau bado hawajaafikiana iwapo sheria hiyo itatumika pia wakati wa kivumbi cha Euro ambacho sasa kimeahirishwa hadi 2021 kwa sababu ya ugonjwa wa Covid-19.

Pep Guardiola wa Manchester City, Jurgen Klopp wa Liverpool na Frank Lampard wa Chelsea ni miongoni mwa wakufunzi wa EPL waliotaka kudumishwa kwa sheria ya kuchezeshwa kwa wanasoka watano wa akiba katika mechi za Ligi Kuu katika msimu wa 2020-21.

Kwa mujibu wa makocha hao, hatua hiyo ingepunguzia wachezaji wepesi wa kupata majeraha mabaya ya mara kwa mara ambayo huwaweka mkekani kwa kipindi kirefu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

STEPHANIE MASEKI: Atumia tajriba ya uigizaji na filamu...

Leeds United wasajili Llorente kutoka Real Sociedad