• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 3:41 PM
USHINDI WA SHIDA: Nigeria yasonga ila mashabiki wahisi udhaifu

USHINDI WA SHIDA: Nigeria yasonga ila mashabiki wahisi udhaifu

Na MASHIRIKA

CAIRO, Misri

HUENDA Nigeria wakaibuka mabingwa wa taji la AFCON la mwaka huu, lakini mashabiki wengi hawajaridhishwa na kiwango cha wachezaji wa sasa wa kikosi hicho ikilinganishwa na nyota wa miaka ya nyuma, timu hiyo ilipokuwa na akina Nwankwo Kanu na Austin ‘JJ’ Okocha.

Baada ya kutinga hatua ya nusu-fainali vijana hao wa kocha Gernot Rohr watakutana na Algeria ambayo ilishinda Ivory Coast katika mechi ya Alhamisi ambapo walitoka sare 1-1 kisha Dessert Foxes wakashinda katika penalti.

Mashabiki wengi hawakuwatarajia kupiga hatua kubwa katika mashindano ya mwaka 2019, lakini baada ya ushindi dhidi ya Cameroon na baadaye Afrika Kusini, matumaini yameanza kurejea.

Mechi dhidi ya Afrika Kusini, ilibidi vigogo hao wasubiri hadi dakika ya mwisho kufunga bao la ushindi.

Hata hivyo, kocha Rohr amewatetea vijana wake akidai muhimu katika mechi ni ushindi hata kama timu haijacheza vizuri.

“Timu haiwezi kucheza vizuri katika mechi zote. Nawapongeza kwa ushindi.”

Kwa upande mwingine, Stuart Baxter wa kikosi cha Afrika Kusini alisema walikuwa na bahati mbaya siku hiyo, siku chache tu baada ya kucheza vizuri dhidi ya wenyeji, Misri na kushinda 1-0.

Mashabiki wamesema Nigeria ya sasa haina wachezaji wa vipaji vya akina Sunday Oliseh, Jay-Jay Okocha na Nwankwo Kanu. Nyota pekee wa kiwango cha juu katika kikosi cha sasa ni kiungo Mikel John Obi, lakini amekuwa akiwekwa katika kikosi cha akiba baada ya kuanza kwenye mechi mbili za kwanza dhidi ya Burundi na baadaye Madagascar, ingawa amekuwa akipewa nafasi kuzungumza na wachezaji wakati wa mapumziko.

Staa huyo wa zamani wa Chelsea aliyecheza kwenye michuano hii kwa mara ya kwanza mnamo 2006 ni miongoni mwa watu wanaoitarajia Nigeria kufuzu kwa fainali na hata kubeba ubingwa wa mwaka huu.

Vilevile, michuano ya mwaka huu imeshuhudia timu kadhaa kubwa ikiwemo Cameroon zikibanduliwa nje mapema na timu limbukeni baada ya kukosa wachezaji wa vipaji vya hali ya juu kama nyakati za akina Njitap Geremi, Rigobert Song na Patrick Mbomba ama Misri ambayo inawakosa wachezaji kwa viwango vya akina Ahmed Hassan, Hosny Abd Rabo na Mohamed Aboutrika.

Kushindwa kufuzu

Kadhalika timu nyingi zikiwemo Burkina Faso, Cape Verde na Gabon zinakosekana hapa baada ya kushindwa kufuzu.

Senegal hawajafaulu hata mara moja kutwaa taji hili lakini kocha wao, Cisse amesema wakati wao umefika.

Walifanya vyema zaidi mnamo 2002 walipomaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Cameroon, lakini timu za Benin na Madagascar zilishangaza wengi kwa kuangusha timu kubwa njiani.

Benin walishangaza jinsi walivyoonyesha mechi zuri dhidi ya Morocco na kumaliza muda wa kawaida wa dakika 90 mambo yakiwa 0-0 kabla ya vijana hao kushinda kwa mikwaju ya penalti.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa timu hiyo kutinga hatua ya robo-fainali, lakini mara ya nne kushiriki katika michuano hiyo. Walishinda Morocco kwa mbaoa 4-1 mbele ya mashabiki waliokuwa wamejaa pomoni.

Walifunga penalti zao kupitia kwa Olivier Verdon, David Djilgla, Ridjani Anaane na Mama Seibou.

  • Tags

You can share this post!

Sababu ya Safaricom kukawia kuzima nambari za malipo za...

Ajuza, 83 akiri kuwa na misokoto ya bangi

adminleo