Video ya busu la pembeni msumari moto kwa Asbel Kiprop
Na Geoffrey Anene
MASAIBU ya Asbel Kiprop yanaonekana kuongezeka Agosti 27, 2018 baada ya video yake akibusu na kupapasa mwanamke mmoja katika gari lake, ambaye sasa anasemekana kunywa sumu.
Vyombo kadhaa vya habari nchini Kenya vimesema Kiprop, ambaye alistaafu kutoka riadha baada ya kushindwa kusafisha jina lake kutokana na matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku kupata ufanisi mashindanoni, alidai kwamba mwanamke huyo alimharibia nyumba yake pamoja na taaluma yake ya ukimbiaji.
Tovuti kadhaa zimesema kwamba Kiprop anadai kwamba mwanamke huyo kwenye video “hutembea” na watu wengi wakiwemo wanariadha watajika “ambao hawezi kutaja.”
Awali, Kiprop alionekana kwenye video hiyo akipapasa mwanamke huyo kifuani na kumbusu, video ambayo imezungumziwa sana na Wakenya na watu wanaofahamu bingwa huyu mara tatu wa dunia wa mbio za mita 1,500 aliyepigwa marufuku mwezi Mei mwaka 2018 kushiriki mashindano yoyote baada ya kupatikana mtumiaji wa dawa za kusisimua misuli.
Kiprop anaonekana akichukua video hiyo akiwa na mwanamke huyo wakisikiza muziki wa Kikalenjin. Mwanamke huyo amefungua blauzi yake na kusalia na sidiria, huku akicheza kiuno chake.
Video hiyo inakamilika na wawili hawa kubusiana, huku Kiprop akielekeza mkono wake wa kushoto kwenye kifua chake na kutumia mkono wa kulia kuchukua video hiyo.
Ripoti zinasema kwamba mwanamke huyo alijaribu kuwania wadhifa wa Mwakilishi wa Wadi katika kaunti ya Uasn Gishu. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa Twitter wameweza kutambua mwanamke huyo, ambaye wanadai ameolewa na aliyekuwa mwekaji kasi wa Kiprop, Andre Rotich. Mwanamke huyo anasemekana amekimbizwa katika hospitali moja mjini Eldoret kupata matibabu baada ya kunywa sumu.
Asbel ana bibi kwa jina Sammary Cherotich na wamejaliwa na mtoto Emmanuel Kiprop.