Michezo

Wakenya wawika Napoli City Half Marathon

February 24th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na GEOFFREY ANENE

WAKENYA Henry Rono na Viola Cheptoo walifagia mataji ya mbio za kilomita 21 kwa rekodi mpya ya Napoli City Half Marathon nchini Italia mnamo Februari 23, 2020.

Rono aliongoza Wakenya wenzake Abel Kipchumba na Evans Kipkorir Cheruiyot kunyakua nafasi tatu za kwanza katika kitengo cha wanaume kwa saa 1:00:04, 1:00:35 na 1:00:42, mtawalia.

Ni mara ya kwanza mwanamume kutoka Kenya alishinda kitengo hiki tangu Cleophas Ngetich atambe mwaka 2015 kwa saa 1:02:41. Muda wa Rono pia ni rekodi mpya ya Napoli City Half Marathon ya wanaume. Alifuta rekodi ya 1:02:09 ambayo raia wa Eritrea Nguse Amlosom aliweka mwaka 2019.

Cheptoo, ambaye pia ni Mkenya wa kwanza kutwaa taji la kinadada tangu Zipporah Chebet mwaka 2015, pia ni mshikilizi mpya wa rekodi ya wanawake ya Napoli City Half Marathon. Alitimka umbali huo kwa saa 1:06:47 akifuta ile ya saa 1:09:53 ambayo mshindi wa mwaka 2019 Angela Jemesunde Tanui kutoka Kenya, aliweka.

Matokeo ya Februari 23, 2020:

Napoli City Half Marathon

Wanaume

Rono Henry (Kenya) saa 1:00:04

Kipchumba Abel (Kenya) 1:00:35

Cheruiyot Evans Kipkorir (Kenya) 1:00:42

Dirirsa Duguma Teshome (Ethiopia) 1:01:10

Koech Meshack Kiprop (Kenya) 1:01:32

Kipleting Edwin (Kenya) 1:01:56

Mutai Abel Kipkirui (Kenya) 1:01:57

Chumo Josphat Kiptoo (Kenya) 1:03:20

Keror Rodgers Kipyego (Kenya) 1:03:22

Fosti Roman (Estonia) 1:05:23

Wanawake

Cheptoo Viola (Kenya) saa 1:06:47

Adhena Gidey Birho (Ethiopia) 1:07:57

Xaba Dimakatso Glenrose (Afrika Kusini) 1:09:30

Cherono Judith (Kenya) 1:11:06

Kiptoo Gladys Jeruto (Kenya) 1:11:30

Mircheva Militsa (Bulgaria) 1:11:43

Konigstein Fabienne (Ujerumani) 1:14:03

Strahl Martina Brigitte (Uswizi) 1:14:13

Console Rosalba (Italia) 1:17:11

Bianchi Maria Grazzia (Italia) 1:20:52

Sevilla Marathon

Wanaume

Mekuant Ayene Gebre (Ethiopia) saa 2:04:46

Barnabas Kiptum (Kenya) 2:05:05

Regasa Bejiga (Ethiopia) 2:06:24

Wanawake

Juliet Chekwel (Uganda) saa 2:23:13

Gada Bontu (Ethiopia) 2:23:39

Sifan Melaku (Ethiopia) 2:23:49

Josephine Chepkoech (Kenya) 2:24:14