• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 10:48 AM
Walusimbi sasa ni kifaa rasmi cha Kaizer Chiefs

Walusimbi sasa ni kifaa rasmi cha Kaizer Chiefs

NA CECIL ODONGO

MLINZI wa Gor Mahia Godfrey Walusimbi hatimaye amejiunga na mibabe wa soka nchini Afrika Kusini, Kaizer Chiefs baada ya uhamisho huo kurasimishwa katika akaunti ya Twitter ya mabingwa hao watetezi wa KPL.

Kaizer Chiefs wamekuwa wakitafuta huduma za sogora huyo huku Gor Mahia awali wakishikilia kwamba mchezaji huyo alikosa kufuata utaratibu unaostahiki kabla ya kuanza mazungumzo na washiriki hao wa ligi ya Absa.

Raia huyo mganda  amekuwa tegemeo kwa kikosi cha vijana wa kocha Dylan Kerr katika mechi za ligi na zile za kuwania ubingwa wa Kombe la Mashirikisho Barani (CAF).

Vile vile, Walusimbi amekuwa mwiba katika kusaidia kuzalisha magoli kambini mwa K’Ogalo, akiwa amechangia mara sita magoli yaliyofungwa na mabingwa hao mara 16 katika mashindano ya CAF ikiwemo katika mechi dhidi ya Yanga SC mwezi Julai waliyoishinda 3-2.

Difenda huyo pia amewahi kukumbwa na misukosuko kati yake na waajiri wake kuhusu kuongezewa mshahara na maswala yanayohusiana na mkataba.

Hayo yalichangia mwanadimba huyo  kukosa  kushiriki mechi za kufuzu kuwania  klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia mwezi Machi, 2018.

Kwa upande wao, Kaizer Chiefs wameanza ligi vibaya msimu huu, wakiwa wamepata alama moja  katika mechi mbili walizoshiriki. Kwa sasa wanashikilia nafasi ya nne katika msimamo wa jedwali la ligi ya Absa iliyoanza Agosti 3 na kushirikisha timu 16.

You can share this post!

Wambora alivyoponea tena mahakamani

Vivo Energy yapunguza bei ya mafuta kwa Sh13

adminleo