Yaya Toure sasa ataka kurithi wajane wa mwendazake Cheick Tiote
Na CHRIS ADUNGO
HATUA ya mwanasoka Yaya Toure kuwania fursa ya kuwarithi wajane wa aliyekuwa kiungo wa Newcastle United na timu ya taifa ya Ivory Coast, Cheick Tiote, imezua mzozo mkubwa.
Toure aliwahi pia kutikisa pakubwa uthabiti wa ndoa kati yake na mrembo Gineba kutokana na jicho kali la nje lililomwelekeza kwa hawara Sandra Ntoya aliyekuwa akimtoza kima cha Sh50,000 kwa kila saa moja ya huduma za chumbani.
Sasa sogora huyo wa zamani wa Barcelona na Manchester City anayechezea Qingdao Huanghai ya China amefichua azma ya kurithi wajane wa Tiote aliyefariki mnamo 2017 akivalia jezi za kikosi cha Beijing Enterprises nchini China.
Kwa mujibu wa magazeti mengi ya udaku nchini Ivory Coast, Toure amekuwa akinyemelea penzi la Madah, mke wa kwanza wa Tiote. Ingawa wazazi wa Madah wameikemea pakubwa hatua hiyo ya Toure ya kuliwania buyu la asali la mwana wao, wazazi wa Tiote wameonekana kuunga mkono juhudi za Toure kiasi cha kumpendekezea pia kumrithi mke wa pili wa marehemu mwanao, Doukrou Laeticia, 34.
Hata hivyo, Toure, 37, ambaye hajaonekana kuvutiwa na Doukrou, amekiri kudondoshwa mate na Madah na aliyekua ‘mpango wa kando’ wa Tiote, Nkosiphile Mpofu kutokana na ukubwa wa ghuba zao.
“Toure ameonekana kupata hifadhi mpya ya penzi lake katika nyoyo za wajane wa Tiote baada ya kukiri kuteswa hisia na urembo wa Madah na Nkosiphile. Hili limekoroga nyongo Gineba kwa mara nyingine na sioni kitakachomzuia kuomba talaka mara hii,” ikasema sehemu ya taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia ya Toure na kunukuliwa na gazeti la The Weekly Guardian nchini Ivory Coast.