Ikuu Girls High School Chuka, Tharaka Nithi
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Ikuu Girls iliyoko Kaunti ya Tharaka Nithi wakifurahia kupigwa picha wakati wa hamasisho la mradi wa Newspapers in Education (NiE). PICHA| CHRIS ADUNGO
Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Ikuu Girls wakichangamkia maswali ya chemshabongo wakati wa hamasisho la NiE. PICHA| CHRIS ADUNGO
Afisa wa mauzo wa Nation Media Group (NMG), Bw Nicholas Muli, akimtuza mwanafunzi shati-tao la Taifa Leo baada ya kujibu swali la chemshabongo ipasavyo wakati wa hamasisho la NiE. PICHA| CHRIS ADUNGO
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Upili ya Ikuu Girls, Bi Elizabeth Mugambi, akipekua safu mbalimbali gazetini. PICHA| CHRIS ADUNGO
Baadhi ya walimu wa Shule ya Upili ya Ikuu Girls wakisoma nakala zao za magazeti siku ya kuzinduliwa rasmi kwa mradi wa Newspapers in Education (NiE). PICHA| CHRIS ADUNGO
Baadhi ya wanafunzi waliotuzwa kofia na kalamu kwa kujibu maswali kwa usahihi wakati wa hamasisho la NiE wakifurahia kupigwa picha ya pamoja. PICHA| CHRIS ADUNGO