• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
TAHARIRI: Washukiwa wa ufisadi hawafai kuingia ofisini

TAHARIRI: Washukiwa wa ufisadi hawafai kuingia ofisini

NA MHARIRI

Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi anataka bunge libuni sheria ambayo itawafanya maafisa wa serikali watakaoshtakiwa kuhusu ufisadi waondoke ofisini.

Wandayi alisema kwamba sheria haijabainisha wazi kinachopaswa kufanywa maafisa kama vile magavana wakishtakiwa kwa ufisadi.

Pendekezo lake laja wakati mwafaka, wakati ambao magavana wanapanga kukata rufaa kortini kupinga agizo la korti kuwazuia magavana Waititu wa Kiambu na Lenolkulal wa Samburu kuingia ofisini mwao hadi kesi za ufisadi zinazowakumba zichunguzwe kwa ukamilifu.

Mahakama iliamuru kwamba kuruhusu Waititu kuhudumia wakazi anaotuhumiwa kuwadhulumu si haki kwao.

Jaji Mumbi Ngugi alimzuia Gavana Lenolkulal kuingia ofisini akisisitiza kwamba si sawa aendelee kuhudumia wakazi wa Samburu anaodaiwa kuwaibia pesa zao.

Haya ni maamuzi mazuri. Maafisa wote wa serikali kuu na kaunti hawana budi kuzuiwa kuingia ofisini iwapo watashtakiwa kwa tuhuma za ufisadi. Hayo ndio yanayowaandama maafisa wa serikali wanaoshtakiwa kwa ufisadi.

Aliyekuwa Waziri wa Fedha Henry Rotich na Katibu wa Hazina ya Kitaifa Kamau Thugge walisimamishwa kazi baada ya kushtakiwa kwa tuhuma za ufisadi.

Zaidi ya maafisa 70 wa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru wameshtakiwa kuhusiana na ufisadi majuzi sasa wamezuiwa kuingia ofisini, kwa maana kwamba kazi yao imesimama kwa muda.

Wengine wengi ambao wameshtakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi na ufisadi kama vile NYS na Kenya Power pia wamesimamishwa kazi. Kwani magavana hawa ni kina nani?

Wao wanasema kwamba kwa vile walichaguliwa na wananchi wa kawaida, wanaweza kufanya chochote watakacho, almuradi hawataguswa. Wananukuu kipengee cha sheria kwamba ‘huna hatia hadi pawe na ushahidi’.

Ufisadi ni uhalifu mkubwa na adhabu yake inapaswa pia kuwa kubwa bila kubagua mtendaji.

Unaua wakati pesa za kununua dawa za hospitali zimefujwa na wagonjwa wanataabika juu ya tiba. Unaua wakati pesa za kununua chakula kama mahindi kwa raia zinaibwa na hakuna anayekamatwa kwa hilo.

You can share this post!

Bwana harusi akata tamaa ya kuishi baada ya mlipuko kuwaua...

Wanaounganishia raia umeme kwa njia za mkato waonywa

adminleo