• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:03 AM
Waluke alakiwa kishujaa bungeni baada ya kukwepa kupoteza ubunge wake

Waluke alakiwa kishujaa bungeni baada ya kukwepa kupoteza ubunge wake

Na Charles Wasonga

MBUNGE wa Sirisia John Waluke Alhamisi alilakiwa bungeni kwa shangwe na nderemo aliporejelea kwa mara ya kwanza, baada ya kuachiliwa kwa dhamana ya Sh10 milioni Jumatatu.

Mbunge huyo ambaye amekuwa gerezani kwa miezi minne aliachiliwa na Mahakama Kuu baada ya kukata rufaa dhidi ya kifungo cha miaka 64, alichopewa kwa shtaka la kupora Sh297 milioni za Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao (NCPB).

Endapo angesalia gerezani kwa miezi sita Bw Waluke angepoteza kiti chake cha ubunge. Alishukuru wabunge, wakazi wa Sirisia na wananchi kusimama naye akisisitiza hana hatia.Mbunge Maalum David Ole Sankok alivunja kanuni za Bunge kupiga makofi kumkaribisha.

“Haufai kupiga makofi, unajua unavyopasa kudhihirisha kwamba wafurahishwa na jambo,” akasema Spika wa muda Jessica Mbalu.Bw Sankok ambaye ni mlemavu alijtetea: “Mheshimiwa Spika unafahamu sina miguu; sharti nioneshe furaha yangu kwa kutumia mikono na mdomo.”

Bw Waluke alishukuru wabunge wenzake, wakazi wa Sirisia na wananchi kwa kusimama naye akisisitiza hana hatia. wakati mgumu akasisitiza hana hatia.

 

You can share this post!

Nilistaafu NMG kwa hiari yangu, asema Lolani Kalu

Wakazi Mombasa watisha kuishtaki serikali kwa kuwafungia