Habari za Kitaifa

Supkem: Waislamu eneo la Pwani wamuunga Ole Naado

January 30th, 2024 1 min read

NA KNA

VIONGOZI wa baraza Kuu la Waislamu nchini (Supkem) eneo la Pwani wameapa kusimama na mwenyekiti wa baraza hilo Hassan ole Naado.

Wanasema kiongozi huyo alichaguliwa na wajumbe kutoka kaunti zote 47 miaka mitatu iliyopita.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza hilo tawi la Mombasa, Athman Akbar, waliapa kusimama na Sheikh ole Naado, walipomkataa Bw Yusuf Nzibo.

“Mwaka wa 2020, wajumbe wote walikataa uongozi wa Bw Nzibo. Alienda mahakamani kupinga uamuzi huo na kupoteza kesi. Kwa nini msajili wa vyama atulazimishe?” akauliza Bw Akbar.