• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Afisa adai aliadhibiwa kwa kutopelekea Ruto umati

Afisa adai aliadhibiwa kwa kutopelekea Ruto umati

Na BRIAN OCHARO

MSIMAMIZI wa wadi katika Kaunti ya Mombasa, Bw Fredrick Otieno, ameambia mahakama anaadhibiwa kwa kukosa kuandaa mkutano wa Naibu Rais William Ruto.

Katika stakabadhi alizowasilisha kwa Mahakama ya Leba Mombasa, msimamizi huyo wa wadi ya Kipevu anadai kuwa alisimamishwa kazi kwa muda bila mshahara akisingiziwa kwa ubadhirifu na utumizi mbaya wa mamlaka.

Korti imeagiza aendelee kulipwa mshahara hadi kesi itakamilika.Katika barua ya kumsimamisha kazi, Bw Otieno anadaiwa kutumia vibaya Sh270,000 na kumkosea heshima Diwani wa Kipevu, Bi Faith Mwende.

Hali kadhalika, anadaiwa kumiliki kitambulisho ghushi cha ajira ya bungeni na kutowashirikisha madiwani katika ulipaji madeni yanayodaiwa na wauzaji bidhaa.

Bw Otieno alimshtaki Bi Mwende, Bodi ya Huduma za Bunge na karani wa Bunge.Alisema bodi na karani wa Bunge walikosa kuingilia kati kukomesha dhuluma alizotendewa na Bi Mwende.

Aliripoti kesi hiyo baada ya Bi Mwende kumwamrisha atoke ofisini mwake na hata kubadilisha kufuli ya mlango. Faili za korti zinaonyesha wawili hao wamekuwa wakizozania uongozi.

Pia wamekuwa wakivutana kuhusu makao ya kisiasa ya Naibu Rais Dkt Ruto.Hii ni baada ya Bw Otieno kukataa kuhamasisha wananchi wahudhurie mkutano wa kisiasa uliohudhuriwa na wanasisa wa mrengo wa Dkt Ruto.

Dkt Ruto alizuru eneo la Pwani mnamo Februari na kufanya mikutano kadha na wafuasi wake na kujipigia debe kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2022.Mikutano hiyo ilikisiwa kuzima umaarufu wa kinara wa ODM, Raila Odinga, mkoani humo.

“Lengo la MCA ni kuniondoa uongozini, anataka atawale pesa za ofisi na kumweka mwingine katika nafasi yangu,” alisema Bw Otieno.

You can share this post!

Wakili Murgor akana vikali kuwa mkorofi

Kituo cha Walibora hatarini kufifia baada ya kifo chake