• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Afrika Kusini, DR Congo na Angola kati ya vigogo wa soka watakaokosa fainali za AFCON 2022

Afrika Kusini, DR Congo na Angola kati ya vigogo wa soka watakaokosa fainali za AFCON 2022

Na MASHIRIKA

AFRIKA Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) na Angola ni miongoni mwa vigogo wa soka watakaokosa kunogesha fainali zijazo za Kombe la Afrika (AFCON) zitakazoandaliwa nchini Cameroon mnamo 2022.

Bafana Bafana ya Afrika Kusini ilipokezwa na Sudan kichapo cha 2-0 katika mchuano wa mwisho wa Kundi C mnamo Machi 28, matokeo yaliyoshuhudia miamba hao wakiambulia nafasi ya tatu kundini kwa alama 10, mbili nyuma ya nambari mbili Sudan.

Ghana waliowapiga Sao Tome & Principe 3-1 katika mechi nyingine, walidhibiti kilele cha Kundi C kwa pointi 13 huku Sao Tome wakikamilisha kampeni zao bila alama yoyote.

Licha ya kupepeta Gabon 2-0 katika mechi ya mwisho jijini Luanda, Angola walivuta mkia wa Kundi D. Nambari tatu DR Congo waliopiga Gambia 1-0 jijini Kinshasa waliambulia nafasi ya tatu. Gambia na Gabon waliokosa huduma za nahodha wao Pierre-Emerick Aubameyang katika mechi ya mwisho dhidi ya Angola, walifuzu kutoka kundi hilo.

Ushindi kwa Afrika Kusini dhidi ya Ghana ambao ni mabingwa mara nne mnamo Machi 25 ungaliwapa tiketi ya kuelekea Cameroon mwaka ujao. Hata hivyo, mabingwa hao wa AFCON 1996 waliambulia sare ya 1-1 uwanjani FNB na kujiweka katika ulazima wa kushinda Falcons of Jediane ya Sudan kwenye gozi lililowakutanisha katika uwanja wa Al Hilal mjini Omdurman.

Kuchapwa kwa Afrika Kusini kunamaanisha kwamba hii ni mara yao ya tano katika historia kutoshiriki fainali za AFCON na ni mara ya nne tangu watawazwe wafalme wa bara Afrika mnamo 1996. Itakuwa mara ya kwanza tangu 2017 kwa Afrika Kusini kutonogesha fainali za AFCON.

Sudan walifunga mabao yao dhidi ya Afrika Kusini katika kipindi cha kwanza kupitia Saifeldin Maki na Mohammed Abdelrahman; na wanafuzu kwa fainali za AFCON kwa mara ya kwanza tangu 2012.

Ni mara ya tatu kwa kikosi hicho kilichotawazwa mabingwa wa AFCON mnamo 1970 kufuzu kwa kipute hicho walichokishiriki pia mnamo 1976.

Katika Kundi J, Tunisia waliwapiga Equatorial Guinea 2-1 nao Tanzania wakapepeta Libya 1-0. Tunisia na Equatorial Guinea ndio waliofuzu kutoka kundi hilo.

Namibia walipiga viongozi Guinea 2-1 katika Kundi A. Mali ndicho kikosi kingine ambacho kimefuzu kutoka kundi hilo linalojumuisha Chad waliopigwa marufuku na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Uganda kukosa kunogesha fainali za AFCON kwa mara ya kwanza...

Japan waponda Mongolia 14-0 katika mechi ya kufuzu fainali...