• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Balala aachiliwa kwa dhamana

Balala aachiliwa kwa dhamana

NA ALEX KALAMA

MAHAKAMA Kuu ya Malindi mnamo Ijumaa imemuachilia kwa dhamana aliyekuwa Waziri wa Utalii Najib Balala pamoja na wenzake wawili ambao walikuwa wameshtakiwa pamoja katika kesi ya ufujaji wa Sh8.5 bilioni za ujenzi wa Chuo cha Utalii cha Ronald Ngala kilichoko eneo la Vipingo katika Kaunti ya Kilifi.

Wakiwa mbele ya hakimu mkuu James Mwaniki katika mahakama hiyo ya Malindi, watatu hao walikanusha mashtaka yanayowakabili.

Hakimu hiyo amemuachilia Bw Balala kwa bondi ya Sh5 milioni na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au pesa taslimu Sh1 milioni. Pia katibu Leah Adda Gwiyo ameachiliwa kwa dhamana inayofanana na ya Bw Balala.

Naye mhandisi Joseph Odero ameachiliwa kwa bondi ya Sh3 milioni au pesa taslimu Sh800,000.

Upande wa washtakiwa umewakilishwa na mawakili watatu ambao ni Bw Mohammed Balala, Bw Maurice Kilonzo, na Bi Lucky Mnyazi.

Upande wa mashtaka umewakilishwa na Joseph Mwangi.

Afisa wa Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC) aliyeiwakilisha ni Bi Gicheru.

Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 28, 2023.

Hakimu Mwaniki amesema kuwa atatoa mwelekeo zaidi siku hiyo ya kutajwa tena kwa kesi hiyo.

Bw Balala alizaliwa mnamo Septemba 20, 1967. Aliwahi kuwa mbunge wa eneobunge la Mvita katika Kaunti ya Mombasa.

Vile vile, alikuwa kinara wa chama cha Republican Congress Party of Kenya (RC) ambacho kilikuwa sehemu ya vyama vilivyotengeneza muungano wa Jubilee.

  • Tags

You can share this post!

Rais Samia Suluhu avunja bodi ya Tanesco kufuatia kupotea...

Warembo wa tattoo wadai ni vigumu kupata mume

T L